Home MAKALA ‘Tutamwambia mama’ Suala la bima ya Afya kwa watoto halijakaa sawa

‘Tutamwambia mama’ Suala la bima ya Afya kwa watoto halijakaa sawa

Google search engine

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan

‘Tutamwambia mama’

Suala la bima ya Afya kwa watoto halijakaa sawa

Na MWANDISHI WETU

WAKATI Serikali ikihangika kukamilisha muswada wa bima ya afya kwa wote ndani ya Bunge lakini bado kuna jambo halijaa sawa hasa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Kuna mijadala Tanzania kuhusu ustawi wa watoto kiafya kwa zingatio la sekta ya afya nchini humo baada ya kusambaa kwa taarifa ya Mfuko wa Bima ya Afya – NHIF, kufuta bima ya afya kwa watoto, “Toto Afya Kadi.”

Machi 15, 2023 ilitolewa taarifa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ukieleza kwamba unafanya maboresho ya utaratibu wa usajili na huduma kwa watoto waliokuwa wanasajiliwa kupitia utaratibu wa Bima ya Afya ya Toto Afya Kadi kwa lengo la kuwafikia watoto wengi ambao wako nje ya huduma.

Kutokana na maboresho hayo wazazi au walezi wanashauriwa kuwasajili watoto wao kama wategemezi wao kwenye Bima ya Afya au kusajili kupitia shule wanazosoma.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Mtendaji Mkuu wa NHIF, Bernard Konga amefafanua utekelezaji  wa mpango huo ambao umeanza Machi 13, mwaka huu.

Hatua hiyo inatajwa kama njia ya kuongeza wigo wa wanachama katika mfumo wa bima ya afya kuelekea bima ya afya kwa wote na kuhakikisha wanachama katika makundi hayo wanajiunga kama familia au kaya au makundi ya wanafunzi kupitia shule wanazosoma.

Mpango wa Toto Afya Kadi ulianza mwaka 2016 ikiwa na lengo la kuwafikia kundi kubwa la watoto walio chini ya miaka 18 ambao kitakwimu ni zaidi ya nusu ya wananchi wote.

Pamoja na hali hiyo lakini bado kuna changamoto kubwa ya malalamiko na vilio kutoka kwa wananchi kuhusu hatua ya kuzuiwa kwa huduma hiyo ambapo kwa sasa kuna idadi kubwa ya watoto ambao hawana matibabu kutokana na kukosa bima hizo.

Kutokana na hali hiyo lakini bado NHIF pamoja na Wizara ya Afya, bado inawajibu kutoa waraka maalumu kwa wakurugenzi wa halmashauri nchini ili kuwapa maelekezo ya namna walimu wa shule za msingi na Sekondari watakavyoweza kusimamia mfumo huo.

Kwa nini ninasema hivyo maana hadi sasa bado kuna danadana ya nani anawajibu wa kuandikisha watoto hao ili waweze kupata bima za afya kama ilivyokuwa awali, maana wakiulizwa walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa shule nao majibu yao huwa ni mepesi kwamba hawawezi kulifanya hilo kwa sababu hawana maelekezo ya kina kuhusu mfumo huo mpya.

Licha ya danadana hizo ni wazi NHIF inaonekana wazi sasa inataka kuwaangamiza watoto hasa wale walikuwa wakionwa na madaktari kupitia bima hizo lakini hatua hiyo sasa imewafanya wakosema huduma ikiwamo hata kupata huduma roborobo kwa kutegemea mfuko wa fedha ya mzazi.

Lakini pia wapi wapo watoto ambao wanaugua maradhi mazito kama ya moyo ambao kupitia bima walikuwa kwenye foleni za upasuaji wa lakini hatua hiyo ni wazi inakwenda kuwanyonga polepole huku wakilichungulia kaburi kwa kukosa huduma stahiki.

Toto Afya Kadi ni kifurushi maalumu ambayo watoto walipatiwa huduma kwa mwaka mmoja kwa gharama ya Sh 50, 400 lakini kutokana na maboresho mfumo huo umesitishwa.

Ni kweli taarifa hiyo ya NHIF ilikuwa haijaweka bayana kuwa huduma hiyo imesitishwa kwa muda gani, uamuzi huo ni kinyume cha kifungu cha 8 cha Sheria ya Mtoto No 21 ya 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 ibara ya 24 ya mkataba wa Kimataifa wa Haki za mtoto 1989 na ibara ya 14 ya mkatana wa Afrika wa haki na ustawi wa mtoto 1989.

Serikali ya Rais Samia imekuwa ikipambana kuhakikisha inafanya mapitio na maboresho kuhusu la bima ya afya kwa watanzania wote lakini kama watanzania tuna wajibu wa kujua mchakato huo umekwama wapi na kwa nini umekuja na kuumiza afya za watoto ambao tunategemea ndio watakuja kuwa viongozi wa baadae.

Leo katika safu hii ya ‘Tutamwambia mama’ tumeona tupaze sauti kwa mamlaka husika ili zigeukie jambo hili na kwenda kuona namna watoto wanavyohangika kwa wazazi wao kukosa fedha mfukoni za kuwatibu kutokana na kukosa bima ya afya.

Ni lazima wabunge sasa kupitia Bunge linaloendelea mjini Dodoma waihoji Serikali hatima ya jambo hili na namna watoto wanavyohangika kukosa matibabu kwa kukosa bima za afya.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here