Home KITAIFA Majaliwa asisitiza matumizi Takwimu za Sensa maandalizi ya Dira ya Maendeleo 2050

Majaliwa asisitiza matumizi Takwimu za Sensa maandalizi ya Dira ya Maendeleo 2050

Google search engine

Na Mwandishi Wetu

-BEST MEDIA, ZANZIBAR

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa Majaliwa amesema ni vyema kutumia takwimu za Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika Maandalizi ya Dira ya Maendeleo ya mwaka 2050.

Mhe. Majaliwa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa ripoti za matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2023 iliyofanyika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema Dira hiyo ni muhimu kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho ambapo matumizi ya Matokeo hayo yatarahisisha kukamilika kwa mpango huo.

Aidha Majaliwa amesema Serikali imejipanga kukukusanya maoni kwa wananchi ili kukamilika Dira hiyo ambapo amewataka kujitokeza kwa wingi ili kufikia lengo la kuwa na Mpango bora na jumuishi.

Aidha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema Matokeo ya Sensa ya watu na makazi yameonesha kupungua kasi ya uhamiaji kutoka Vijijini kwenda Mijini kutoka Asilimi 5.2 kwa mwaka 2002 mpaka 2012 na kufikia Asilimia 4.8 kwa mwaka 2012 hadi 2022 hatua ambayo inatokana na juhudi za Serikali kufikisha huduma mbali mbali za kijamii vijijini ikiwemo huduma za Afya, Elimu, huduma za kiuchumi na kupunguza umasikini wa kipato kwa maeneo yote.

Sambamba na hayo, Majawali amewataka wadau na wananchi kufuatilia taarifa za matokeo hayo kwa ukaribu na kuyatumia katika kufanya maamuzi mbali mbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kubaini maeneo ya uwekezaji, upatikanaji wa huduma za kijamii na maeneo ya masoko kulingana na mgawanyiko wa Idadi ya watu nchini.

Aidha Mhe. Majaliwa amewashukuru washirika wa maendeleo kwa kuunga mkono Sensa ya mwaka 2022 na kueleza kuwa hiyo ni ishara ya ushirikiano mzuri baina yao na Serikali kwa mustakabali mzuri wa Tanzania.

Nae Mwenyekiti mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi, Hemed Suleiman Abdulla amesisitiza Wizara za Fedha Nchini kuzingatia takwimu hizo katika uandaaji wa bajeti hasa katika kupanga mipango ya maendeleo Nchini.

Aidha Hemed amezishukuru Serikali za Mikoa Nchini kwa kuwa sehemu kubwa ya kukamilisha Sensa hiyo ambapo ushiriki wao umeweza kusaidia makarani na maafisa kuyafikia maeneo husika kwa urahisi zaidi.

Aidha Mhe. Hemed ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameyashukuru makundi yote kufanikisha kwa Asilimia kubwa kwa kuhakikisha Sensa hiyo inafanikiwa vizuri

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, Sera, Bunge na uratibu, Jenista Muhagama ameeleza kuwa matokeo ya Sensa ya watu na makazi Zanzibar ya mwaka 2022 ni nyenzo ya kujenga ustawi mzuri wa watanzania na maendeleo kwa ujumla.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here