Home KITAIFA Mfumo usaili ajira kielektroniki serikalini sasa waiva

Mfumo usaili ajira kielektroniki serikalini sasa waiva

Google search engine

Na Mwandishi Wetu

-BEST MEDIA, MWANZA

Mfumo wa usaili kielektroniki kwa waombaji ajira serikalini, utaanza kutumika mwanzoni mwa mwaka ujao wa fedha, ili kumuwezesha kila mmoja kushiriki akiwa katika mkoa wake.

Mfumo huo umelenga kupunguza, pamoja na mambo mengine, usumbufu na gharama wanazoingia waombaji kwa kulazimika kukusanyika siku kadhaa makao makuu ya nchi kwa mchakato wa usaili.

Hayo yamesemwa leo Aprili 24,2023 jijini Mwanza na Naibu Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Samwel Tanguye, ambapo amesema katika mkutano wa ukusanyaji maoni kwa ajili ya kuboresha kanuni za uendeshaji wa shughuli za Sekretarieti.

Amesema baadhi ya vyuo vya kati, ikiwemo vya ufundi na vya elimu ya juu kila mkoa, vyenye maabara ya kompyuta vitatumika kufanya usaili wa awali ambao ni wa kuandika.

“Sekretarieti itaunganisha mfumo kwenye maabara hizo. Itakua ikituma maswali wakati huohuo wa usaili katika chuo husika, ambapo mwombaji ajira atapata majibu yake hapohapo.

“Watakaopita katika mchujo wa kwanza ndio watakaolazimika kusafiri kwenda Dodoma kwa ajili ya usaili wa mdomo. Tunafanya hivi ili kila mwenye sifa apate nafasi, bila kujali anatoka kwenye familia ya hali gani,” amesema.

Kwa maoni yake Diwani wa Kata ya Bujora wilayani Magu, Bunyanya John, amesema utaratibu uliopo sasa wa uwepo wa nafasi moja tu ya ajira, lakini wanaitwa waombaji zaidi ya hata 500 sio sawa, akaishauri sekretarieti kurekebisha jambo hilo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here