Home KITAIFA Pinda asisitiza teknolojia zitakazosaidia wafugaji nchini

Pinda asisitiza teknolojia zitakazosaidia wafugaji nchini

Google search engine

Na Mwandishi Wetu

-Tanga

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Kilimo Tanzania, amevishauri vituo vya utafiti wa mifugo kuja na teknolojia zitakazosaidia wafugaji kupata mazao bora, ambayo yatauzika kwa urahisi na hivyo kukuza vipato vyao.

Ushauri huo ameutoa leo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea mpango wa mifugo bora kwa maisha bora na fursa za ajira kwa vijana katika vituo vya Buhuri na TALIRI mkoani Tanga.

Amesema Tanzania ina utajiri mkubwa wa mifugo, lakini bado sekta hiyo imekuwa ina mchango mdogo katika pato la Taifa, hivyo amewataka wataalamu kuhakikisha wanakuja na teknolojia rafiki, ambazo zitawasaidia wafugaji kufunga kisasa, lakini kupata mazao mengi yenye ubora.

“Dhamira ya Rais Samia ya mpango wa kuweka vituo atamizi, ili vijana waweze kujifunza ni njia mojawapo ambayo si tu itamaliza changamoto ya ajira, bali itatoa fursa ya kuweza kujiajiri na kuimarisha kipato chao na uchumi wa nchi,”amesema Pinda.

Naye Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde amesema kuwa dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona sekta hiyo inachangia pato la Taifa zaidi ya asilimia 10 tofauti na sasa.

“Mpango huu wa mafunzo ya ufugaji kwa vijana umeweza kuwafikia takribani vijana 240 nchi nzima kwa awamu ya kwanza, ambapo watafundishwa mbinu za ufugaji sambamba na kupewa mitaji kwa ajili ya kujiendeleza,”amesema Naibu Waziri huyo.

Nae Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI),  Profesa Erick Komba amesema kuwa kati ya wahitimu wa elimu ya juu 2000 ambao wanamaliza vyuo kila mwaka ni asilimia 9.5 pekee ndio wanaajiriwa na sekta hiyo.

Hivyo kupitia mpango huo wataalamu wanaomaliza vyuo vikuu hapa nchini, wataweza kupata fursa ya kutumia utaalamu wao kuweza kujiajiri na hivyo kuchangia Pato la Taifa.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here