Home MAKALA ‘Tutamwambia mama’ Hili linalofanywa Slipway Hoteli hakika wanakuchezea

‘Tutamwambia mama’ Hili linalofanywa Slipway Hoteli hakika wanakuchezea

Google search engine

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan

‘Tutamwambia mama’

Hili linalofanywa Slipway Hoteli hakika wanakuchezea

Na Mwandishi Wetu

-Dar es Salaam

Ama kweli ukistaabu ya Mussa utayaona ya Songoro Mnyonge. Ndivyo unaweza kusema hasa kutokana na jambo zito ambalo limepata kuibuliwa Aprili 27, 2023 ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Tanzania ni nchi iliyobarikiwa maliasili nyingi sana ukilinganisha na nchi nyingine. Tumebarikiwa madini aina mbalimbali  kama vile dhahabu(Geita), almasi(Mwadui-Shinyanga), makaa ya  mawe(Kiwira), na madini yasiyopatikana sehemu yoyote ile duniani, Tanzanite. Ukiachana na madini, pia Tanzania ina  wanyama wengi wa kuvutia kama vile; simba wanaopanda miti,vyura wanaozaa(Kihansi) nk.

Tofauti na nchi nyingine ambazo suala la upatikanaji wa vyanzo vya maji ni tatizo hasa kwa ajili ya shughuli za kiuchumi kama Zambia (land locked country), Tanzania imejaaliwa mito, maziwa na bahari. Kando kando mwa maziwa na bahari kuna fukwe ambazo ni hazina kubwa ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu.

Moja kati ya lililoibuliwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Comredi Songoro Mnyonge ambapo naomba kunukuu;

“Ndugu zangu leo tumekuja hapa kwenye ziara tukiwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi ya Manispaa ya Kinondoni, kufutilia mgogoro baina ya Halmashauri ya Kinondoni na mmiliki wa Hoteli ya Slipway.

“Mgogoro huu umetokana na ukweli kwamba halmashauri  imebaini bil shaka kuna mchezo mchafu umefanyika kupitia wataalamu wa ardhi Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi ya kumuongezea eneo mmiliki wa hoteli ya Slipway.

“Na kwa kumuongezea eneo hilo wamechukua eneo ambalo ni la Serikali bila ya utaratibu bila ya vikao vyovyote na kulitoa eneo hilo kwenye miliki ya Serikali na kusema sasa eneo hilo ni miliki ya mmiliki wa Slipway.

“Eneo ambalo wameingia ndani ya Bahari zaidi ya mita 850 toka mwaka 2004 mmiliki huyo wa Hoteli ya Slipway amekuwa akitambua na amekubaliana na mamlaka halali za serikali kwamba ameingia kwenye eneo la Bahari kwa sababu amejaza kifusi na baada ya kutambua kwamba ameingia kwenye eneo hilo, alikuwa akililipia kwa matumizi ya umma na sisi tulimtaka asiweke Parmanent Structure kwa maana majengo ya kudumu kwa maana eneo lile linatakiwa libaki wazi.

“Toka mwaka 2004 wamekuwa akilipa halmashauri mpaka mwaka 2022, juzi kwa mastaajabu makubwa tumepata taarifa kwa kuja halmashauri na kusema kwamba sasa yeye hatalipa tena ile kodi ambayo alikuwa akilipa halmashauri kwa sababu amepangisha na watu wengine kwenye eneo hili.

“Alidai kwamba eneo hili ameshapewa miliki na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, baada ya kulipokea hili na kulijadili tukaona tuje hapa kwa sababu mchoro tulionao sisi Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni unaonyesha kabisa eneo alilopo si la kwamba lakini tumeshtuka kuona ametengenezewa mchoro mpya ambao unamuhalali kwamba eneo hilo ni lake.

Hata hivyo hili linakwenda kinyume na sheria za nchi kwa sababu hata mawe yake yapo ndani ya Bahari kwa sababu yameingia mita 850 ndani ya bahari  na sheria inasema mtu yoyote ambaye ana plot kwenye bahari anatakiwa ameachia mita 60 lakini mwenzetu hajaachia mita hizo lakini ameingia ndani ya bahari kwa mita 850.

“Sisi kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni tunaiomba Serikali kwanza ifute huo mchoro uliochorwa. Iwafuatilie waliochora kina nani na ulipitishwa na vikao gani kwa sababu kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji mamlaka ya kwanza ya upangaji ni halmashauri husika.

“…Katika kumbukumbu zetu hatujawahi kukaa na kupitisha mabadiliko yam choro wa eneo hili lakini tumeshtuka na kuona kuna mchoro umetengenezwa ambao unampa mamlaka ya uhalali mmiliki wa Slipway kwababu hata hati aliyonayo hajajulimlisha eneo hili,” mwisho wa kunukuu

Ni ukweli usipingika kwamba ‘manyang’au’ ndani ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa miaka mingi wamekuwa kwenye kampeni mbalimbali za kutakatisha upigaji hasa wa maeneo ya wazi huku kwa kiasi kikubwa mate yakiwatoka hasa kando mwa Bahari na Maziwa.

Hili inatokana na hali halisi kwamba upigaji wa viwanja vilivyopo ufukweni vina dili sana hasa kutokana na kupendwa na watu wengi wenye ndoto ya kuendesha biashara ya hoteli na hata utalii.

Vivutio vingi vya fukwe za nchini Tanzania vimekuwa vikitoweka siku hadi siku kutokana na uvamizi wa  wageni lakini hasa unaochagizwa na ongezeko la ujenzi wa hoteli ya kifahari  pembezoni mwa bahari na maziwa.Wamiliki wengi wa hoteli hizi wamekuwa wakijenga kuta kuzunguka hoteli ili kuwazuia wananchi kufika katika fukwe hizi  ambazo ni mali yao ya asili.

Kibaya zaidi hoteli nyingi zimekuwa zikitililisha maji taka na kuyaelekezea baharini na ziwani kama njia rahisi ya kumwaga taka. Kitendo hiki ni hatari kwa afya za wananchi pamoja na mazingira. Nia ya makala hii ni kuelezea faida za fukwe, kwa nini fukwe zinavamiwa , madhara ya uvamizi na nini kifanyike ili kuondokana na tatizo hili.

Wengi watajiuliza nini kinasababisha ongezeko la uvamizi wa fukwe?. Suala la uvamizi wa fukwe nchini Tanzania haliwezi kutenganishwa na ongezeko la rushwa na ufisadi nchini. Maeneo mengi ya wazi na fukwe nchini Tanzania  yamevamiwa hasa maeneo ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam.

Kitendo hiki kinachochewa na vitendo vya rushwa miongoni mwa maofisa wa ardhi, viongozi wa serikali kuu na serikali za mitaa. Ushahidi unaonyesha kuwa watendaji hawa wamekuwa wakipokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa ambao wanayatumia maeneo haya kwa ajili ya ujenzi wa mahoteli ya kitalii (rejea taarifa ya habari iliyorusha siku ya tarehe 19/07/2010 na kituo cha televisheni cha TBC1).Hata hivyo, hili linaweza kuthibitishwa na kitendo cha kupelekwa mahakamani  kwa baadhi ya maofisa ardhi wa wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za uuzaji holela wa maeneo ya wazi na fukwe.

Juni 21, 2015, katika eneo hili ambalo sasa linaibua mgogoro mpya la Hoteli ya Slipway Serikali ilimjia juu mmiliki wa hoteli hiyo na kumtaka kusitisha shughuli zote za ujenzi zinazoendelea pembezoni mwa bahari ya Hindi.

Agizo hilo lilitangazwa na Mwanasheria wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),  Manchare Heche  ambapo alisema kuwa amri hiyo imetoka kwa Waziri wa Mazingira baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi wanaozunguka hotel hiyo.

Walimpa barua hiyo na kumtaka mmiliki huyo kusitisha ujenzi uliokuwa unaendelea katika hoteli hiyo ya kuchukua vifusi na kuingiza baharini ili kupata nafasi kwa kuongeza majengo katika eneo la bahari.

Na endapo atakaidi kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitafuata na kupelekea kuifungia kabisa kwa kutoendelea na huduma za hoteli ndani ya nchi.

“Agizo limetoka kwa waziri ili mmiliki wa hoteli hii aachane na shughuli zote za ujenzi katika eneo hiili kutokana kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira na kuharibu eneo la bahari kwa kujaza mawe na vifusi vya michanga,” alisema Heche.

Ilibainika kwamba mmiliki wa hoteli hiyo anapeleka vifusi pamoja na mawe makubwa katika bahari kwa kutumia katapila pindi maji yanapohama nyakati za asubuhi.

Hatua hiyo iliiing’iniza Slipway kutokana na kukiuka sheria za bahari na wizara kwa kutofuata taratibu na vibali vya kufanya hivyo na kupelekea serikali kutupiwa lawama na wananchi mabazo zinafanywa na watu wachache.

Kama hilo lilibuka wakati huo na hatua zilichukulia kwa mmiliki huyo kwa nini sasa ambapo amefanya jaribiom la hatari la kubadili hatia ya Ardhi kinyume na utaratibu hasa kutokana na eneo hilo kuzuiwa kufanyika hilo kama sheria inavyotaka.

Ni wazi kwamba kolamu hii ya ‘Tutamwambia mama’ inafikia tamati ikiamini kwamba Waziri wa Ardhi, Nyuma na Maendeleo ya Makazi, Dk. Anjelina Mabula atayatakari haya kwa kina badala ya kusubiri mamlaka yake ya uteuzi ifikirie zaidi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here