Na Mwandishi Wetu
-Lindi
Benki ya NMB imetoa msaada wa vitanda na vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh17.5 milioni kwa shule mbili zilizopo wilayani Nachingwea mkoani Lindi.
Shule zilizopata msaada huo ni ya Msingi Kibaoni ambayo imepata vifaa vya ujenzi ambavyo ni mabati, mbao, misumari vyenye thamani ya Sh7.9 milioni na Shule ya Sekondari ya wavulana ya Rugwa iliyopata vitanda vya wanafunzi (double Decker) 44.
Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Roman Degeleki alisema jana wakati wa makabidhiano ya msaada huo kuwa serikali imefanya jitihada kadhaa katika sekta ya elimu lakini hata hivyo bado zipo changamoto mbali mbali hivyo NMB inaungana na serikali kuzitatua.
“Changamoto ni kubwa katika sekta ya elimu hapa Wilayani hii hivyo tumeweka kipaumbele kuhakikisha tunasaidia pale ambapo serikali ilianza” alisema Degeleki.
Benki ya NMB imekuwa ikitoa sehemu ya faida yake kwa jamii katika sekta ya elimu, afya na hivi karibuni mazingira.
Diwani wa Kata ya Chiumbati, Shaibu Rajabu ilipo shule ya Sekondari ya Rugwa aliishuruku NMB kwa msaada na kuema sema kuwa bado zipo changamoto kadhaa kwa sababu kata hiyo ni mpya.
Mkuu wa shule ya msingi Kibaoni, iliyopo kata ya uhalisia madarasa nane inapungukiwa vyumba vitatu vya madarasa, kukosa rasim
Iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Nachinwgea
Rasilimali fedha kupokea msaada utakaowawezesha kufikia malengo ya kuezeka madarasa mawili ya shule ya msingi kibaoni, kupitia msaada huu mliotukabidhi leo, mmetukwamua sisi na Taifa kwa ujumla kupunguza changamoto ya miundombinu ya madarasa ya shule ya msinhi kibaoni na kuondoa changamoto ya wanafunzi kuchanganya madarasa mawili tofauti katika chumba kimoja cha madarasa au kusoema chini ya miti.
Wito kwa wananchi kuanzia kijiji cha kata hii kuendelea kujiunga na benki ya NMB kwani inajali wananchi wake kwa kusaidia vitu mbali mbali
Diwani wa Kata ya Naipingo, ilipo shule ya Msingi kibaoni, Sylvanus Chembe alisema hafla ya makabidhiano kwa niaba ya wananchi wa msaada wa thamani ya Sh7.3 milioni, ni changamoto ilikua inatusumbua muda mrefu, msaada ambao tumeupokea leo,
Si mara ya kwanza kupokea misaada hii tulishapokea viti na vitu vingine mbali mbali
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Chionda Kawawa alisema aliahidi kushirikiana na viongozi wa shule hizo kuvitunza vifaa ili viweze kusaidia wanafunzi wa sasa na wajao.
“Kupitia uuzaji wa mazao kwa stakabadhi ghalani katika mikoa hii yote naomba wana Chiumbati na Nachingwea twendeni tukaiunge mkono NMB kwa kufungua akaunti katika benki hii kwa sababu ni rafiki aliye karibu” Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Adnani Mpyagila.
Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Moyo aliishukuru benki ya NMB kwa msaada na kuwaomba waendelee kuiunga msaada serikali katika sekta ya elimu kama ambavyo wameendelea kufanya
“Yapo majengo mengi tunahitaji, nyumba za walimu, mabweni, maabara tunaomba mtuunge mkono katika shule hii ya mfano” alimalizia mkuu wa wilaya.