Home KITAIFA Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia Bilioni 1.2/-

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia Bilioni 1.2/-

Google search engine
Afisa mkuu wa wateja Wakubwa na Serikali WA Benki ya NMB, Alfred Shao akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni 200 iliyotolewa kwa ajili ya udhamini wa Mkutano wa 37 wa ALAT unaofanyika Arusha . anayepokea hundi ni  Makamu Mwenyekiti wa ALAT, Sima Constatin na wengine ni baadhi ya Maafisa waandamizi wa Benk ya NMB na pia kutoka ALAT, Bw Praygod Mphuru ambaye ni Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya kaskazini ,wa pili kushoto,akifuatiwa na Bi Vicky Bishubo mkuu wa idara ya Biashara za serikali, na wa kwanza kulia ni Zahara Michuzi ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita ,wa pili ni katibu wa ALAT Taifa Mohamed Maje.

Na Mwandishi Wetu

– Arusha

Benki ya NMB imebainisha utayari wake wa kuendelea kufanya kazi kwa karibu na serikali za tawala za mitaa, ikiwemo kufadhili mikutano ya kila mwaka ya Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT).

Dhamira ya kudumisha ushirikiano huo iliwekwa bayana jana jijini Arusha na benki hiyo wakati inatangaza ufadhili wa TZS milioni 200 wa mkutano mkuu wa 37 wa ALAT ambao umeanza rasmi leo hii.

Wakizungumza kabla ya kutangazwa kwa udhamani wa mwaka huu kwenye Ukumbi wa AICC, viongozi waandamizi wa NMB walisema hii ni mara ya saba kwa taasisi yao kufanya hivyo.

Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Alfrded Shao, alisema udhamini walioufanya ndani ya kipind hicho sasa umefikia zaidi ya Sh bilioni 1.2.

“Tuna miaka zaidi ya saba pamoja na ALAT katika masuala ya maendeleo ya taifa letu na ndio maana wenzetu walipotufuata tuwaunge mkono hatukusita hata kidogo,” alibainisha.

“Hata hivyo, kubwa zaidi leo tunatangaza ushiriki wetu kama mdhamini wa Mkutano Mkuu wa ALAT kwa kiasi cha TZS milioni. 200 ilikufanikisha mkutano huu,” aliongeza na kusema wamekuwa wakishirikiana na ALAT hasa kusaidia kuboresha miundombinu ya elimu, afya, usafiri na mazingira kupitia wananchama wake ambao ni halmashauri 184 nchini kote.

Aidha Shao aliitumia hafla ya kukabidhi hundi ya udhamani wa mwaka huu kuonyesha jinsi NMB inavyozihudumia halmashauri, serikali kuu na taifa kwa ujumla hasa kupita huduma zake bunifu za kifedha.

Amesema moja ya maeneo ambayo wamefanikiwa katika hilo ni kurahisisha ukusanyanji wa kodi kupitia mifumo bora inayowezesha Serikali ya Awamu ya Sita katika kukusanya mapato yake.

“Ubunifu na uwekezaji ambao tumeufanya kwenye teknolojia ulituwezesha kuwa benki ya kwanza kuunga mifumo yetu na Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) na hadi sasa zaidi ya taasisi 1,100 tayari zimeunga mifumo yake kwenye mifumo ya NMB ya ukusanyaji wa mapato,” kiongozi huyu alibainisha.

“Kwa mfano, kupitia mifumo yetu mbalimbali ya malipo tumewezesha Serikali kukusanya Shilingi trilioni 8.6 kupitia GePG kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2019 hadi 2021,” aliongeza kusema akisisitiza kuwa fedha hizi zilikusanywa kupitia mifumo ya kidijitali kama NMB Mkononi, NMB Wakala na hata internet banking.

Kauli mbiu ya mkutano mkuu wa ALAT wa mwaka huu ambao ni wa siku tatu ni: “Uboreshaji wa Miundombinu ni Chachu ya Utoaji wa Huduma Bora katika Mamlaka za Serikali za Mitaa”.

Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Sima Costantine Sima, aliipongeza NMB kwa kusaidia kuboresha upatikanaji wa huduma hasa zile za kifedha nchoni lakini pia mchango wake katika kuendeleza ustawi wa jamii.

Amesema ALAT na wananchama wake 184 wanathamini ushirikiano wao mzuri wa kibiashara na kimaendeleo na benkii hiyo ambao umekuwa ni wa manufaa kwa wao wote pamoja na wananchi wanaowahudumia.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here