Home MICHEZO RAIS DK.MWINYI AHUDHURIA UFUNGUZI WA OLIMPIKI MAALUM BERLIN

RAIS DK.MWINYI AHUDHURIA UFUNGUZI WA OLIMPIKI MAALUM BERLIN

Google search engine

Na Mwandishi Maalum

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mkewe Mariam Mwinyi amehudhuria sherehe za ufunguzi wa Mashindano ya Dunia ya Olimpiki Maalumu mwaka 2023 katika uwanja wa Olimpia Jijini Berlin nchini Ujerumani jana tarehe 17 Juni 2023.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoshiriki katika michezo hiyo ikitafuta medali kwenye mpira wa wavu na riadha.

Rais Dk.Mwinyi katika msafara wake ameambatana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Pindi Chana, Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Maulid Mwita,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dk.Abdallah Saleh Possi.

Mashindano hayo yamefunguliwa jana tarehe 17 Juni na kumalizika 25 Juni 2023

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here