NA MWANDISHI WETU
WATANZANIA na wafanyabiashara wenye uwezo wa kununua samaki walengwa wameombwa kununua Samaki kwani kuna nafasi ya kununua tani mia tatu kwaajili ya watanzania.
Hayo ameyasema Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Suleiman Makame jijini Dar es Salaam leo Februari 07, 2023 wakati akizungumza mara baada ya Kushushwa kwa samaki wasiolengwa ili watanzania waweze kula na kufikia lengo la kwa kila mmoja kula samaki kilo 10 hadi 20 zinazotakiwa kuliwa kila mwaka.Amesema watanzania ambao wapo tayari kufanya biashara hiyo kuna… tani mia tatu zinatakiwa kununuliwa ili kuweza kujenga dhamira serikali ya Uchumi wa bBluu na watanzania kuweza kula wanaoshauri kwaajili ya kujenga mwili.
“Kwahiyo watanzania ambao wapo tayari wajitokeze kununua samaki hawa, watu wa usimamizi wa bahari kuu wasimamie hilo ili wale ambao watakuwa na uwezo waweze kununua samaki hao na niombe zoezi hili liwe endelevu.”
Amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Pacific star, Kampuni ya Tuna Ltd na Kampuni tanzu ya Albacora ya nchini Uhispania wameshusha tani 60 za Samaki ambazo walikubalia kuvua kwaajili ya watanzania.
Amesema kuwa katika masharti ya Mkataba wanaweza kuongeza tani hapa nchini ambazo zitakwenda kuwa nufaika watanzania kwenye Chakula.
“Awamu ya kwanza walishusha tani 26, awamu ya pili walishusha tani 25 na leo zimeletwa tani 60 hii ni mali ya serikali Makubaliano yetu yameleta matunda na kuonesha namna uvuvi wa bahari kuu unavyotakiwa kuwa na niwashukuru wenzetu wa Pacific Star kwa kutekeleza ahadi ambayo wameweka.”
Amesema kuwa azima ya Serikali ni kuhakikisha kwamba tunakula samaki ambao wanavuliwa katika bahari yetu. kwa jitihada hizo serikali imeamua kuingia mikataba kampuni mbalimbali kwaajili ya uvuvi wa bahari kuu wapo ambao wanavua kwa leseni maalumu lakini wapo wale ambao wamesajiliwa na Tanzania.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Utafiti na Mafunzo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mohammed Sheikh amesema kupitia ushushaji wa Samaki hao Serikali inahamasisha uwekezaji ili kupata samaki ambao hawakutarajiwa kuvuliwa ili watanzania wapate lishe.
“Watanzania kwasasa tunatumia kilo 8.5 na hizi hazitoshi wenzetu wazanzibar wanatumia kilo 22 kwa Mwaka na wastani wa duniani kila mtu anatakiwa kula kilo 20 za samaki kwa mwaka.”
Pia ameomba watanzania waongeze kula milo yenye samaki ili kuweza kufikia viwango vya kimataifa vya ulaji wa Samaki kwa Mwaka ambapo inatakiwa kila mmoja ale kilo 10.5 ambazo bado ni ndogo hatujafikia kilo ambazo tunatakiwa kula.
Akizungumzia kuhusiana na mikataba Prof. Sheikh amesema kuwa mikataba mizuri ambayo itaiwezesha serikali kupata fedha za kupeleka mbele maendeleo.
Amesema kuwa huwezi kuwa na maendeleo kama hakuna wananchi ambao wanaafya bora kwani Protini ya Samaki ni rahisi kumeng’enywa kwenye mwili.
Amesema kama Wizara wakipata meli zote zilizopewa leseni na kuleta samaki ulaji wa samaki utaongezeka na pato la Taifa litaingezeka na itasaidia katika lishe bora.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu, Emmanuel Sweke amesema kuwa amesema kuwa kampuni hizo zinawajibu wa kulipia vitu vyote serikali ikiwemwo Leseni, Mainjinia na Manahodha pamoja na Kushusha Samaki tone mia Moja kwa Mwaka.
Kupitia ushushwaji wa Samaki hai pia wamekidhi usalama wa Chakula na Lishe kwani mahitaji ya Samaki Tanzania ingawa bado uhitaji ni makubwa kuliko upatikanaji wake.
Amesema samaki hao walioshushwa leo wameuzwa kwa kufuata utaratibu wa Serikali.
Pia katika ushushaji wa Samaki hao wamesaini Mikataba ya makubaliano kwaajili ya kuendelea kuvua samaki katika bahari kuu hapa nchini.
Leseni moja ya katika Uvuvi katika bahari kuu ni dola za Kimarekani elfu sabini (70,000 USD) ambapo mpaka sasa Tanzania imetoa Leseni nne (4) kwa makampuni ya Uvuvi.