Home KITAIFA MAMLAKA ZINAVYOPAMBANA NA MBINU MPYA ZA UJANGILI NCHINI

MAMLAKA ZINAVYOPAMBANA NA MBINU MPYA ZA UJANGILI NCHINI

Google search engine
Ofisa Wanyamapori daraja ya kwanza wa Tawa, Tryphon Kanon alipokuwa akitoa mada kwenye semina ya wahariri iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari wa Mazingira Tanzania (JET) chini ya ufadhili wa mradi wa Tuhifadhi Maliasili unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Meneja ufuatiliaji mradi wa Tuhifadhi Maliasili unaofadhiliwa na USAID, John Noronha, akiwasilisha mada kwa wahariri Mjini Bagamoyo hivi karibuni

NA MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

Ujangili au uwindaji haramu ni tendo la kuwinda wanyama bila kibali au kinyume cha sheria za nchi hii ndio tafsiri ya ujangili.

Kwa milenia nyingi kabla ya kubuniwa kwa kilimo na ufugaji, uwindaji ulikuwa njia ya kawaida kwa watu kujipatia chakula cha nyama.

Tangu kutokea kwa madola au mifumo mingine ya utawala wanyama wa windo walianza kuwa haba katika maeneo kadhaa na hapo watawala walilenga kutunza haki ya kuwinda kwao wenyewe tu. Hii ilikuwa hali ya kawaida katika nchi za Ulaya wakati wa karne za kati.

Mtazamo huo ulipelekwa Afrika wakati wa ukoloni, pamoja na hayo, uwindaji ulionekana kuwa hatari kwa aina za wanyama wenye thamani ya kibiashara, kama vile tembo waliowindwa kwa kulenga ndovu zao. Hata kabla ya ukoloni, tembo walikuwa walipungua katika nchi za Afrika ya Mashariki zilizo karibu na Pwani.

Baada ya uhuru nchi nyingi zililenga kuweka taratibu za uwindaji zilizobana haki za wananchi kuwinda.

Pengine watu maskini wanakimbilia ujangili ili kupata mahitaji yao, lakini mara nyingi zaidi ni waroho ambao wanatafuta faida kubwa inayopatikana kwa njia hiyo, kwa mfano kwa kuua tembo na vifaru ili kunyofoa na hatimaye kuuza pembe zao.

Kutokana na hali hiyo Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa), inaeleza kwamba vifo vinavyotokana na ujangili wa tembo katika maeneo wanayosimamia vimepungua kutoka 50 mwaka 2013 hadi sifuri mwaka 2023.

Akitoa takwimu hizo hivi karibu mjini Bagamoyo Ofisa Wanyamapori daraja ya kwanza wa Tawa, Tryphon Kanon alipokuwa akitoa mada kwenye semina ya wahariri iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari wa Mazingira Tanzania (JET) chini ya ufadhili wa mradi wa Tuhifadhi Maliasili unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Kanon amesema kupungua kwa ujangili, usafirishaji na biashara haramu ya meno ya tembo kunatokana na jitihada za Serikali kwa kushirikiana na wadau ndani na nje ya nchi.

Licha ya hali hiyo amesema biashara ya ujangili inahusisha mnyonyoro wa watu wa ngazi tofauti hivyo hatua za kukabiliana nayo ilihitaji mbinu, rasilimali na vifaa vya kisasa

“Zipo hatua mbalimbali tunazochukua kwa muda mrefu kwenye maeneo ya mapori tengefu na ya akiba ambayo tunasimamia kwa mujibu wa sheria, ikiwamo kuongeza doria katika hifadhi zetu, kuongeza askari wapelelezi waliosaidia kubaini wauzaji wa pembe hizo, tumeshirikisha jamii kuona hili ni tatizo hatari kwa Taifa letu,” amesema kanon

Amesema meno ya tembo yanayokamatwa kwa asilimia kubwa ni yale yaliyofichwa miaka ya nyuma kwa kuwa wanaokamatwa nayo huwaeleza kwa kina walivyoyapata.

Amesema hata hivyo biashara hiyo ilishamiri kutokana na wananchi wanaoishi Jirani na hifadhi kushirikiana na majangili kwa malipo tofauti kulingana na kazi wanazofanya.

“Tulipokuwa tukiwahoji watu tuliokuwa tukiwakamatwa tulibaini kilo moja jino la tembo linauzwa Sh 50,000 mpaka Sh 70,000 ambapo yule anayempiga risasi analipwa 10,000, anayewaongoza na kuwaonyesha njia 5,000, anayeng’oa 10,000 na wabebaji 5,000” amesema

Amesema Tawa kwa kushirikiana na wadau wanaamini elimu sahihi ikitolewa kwa jamii vitendo hivyo vitaondoka kwa watakuwa mstari wa mbele kuwafichua majangili na wanaoshirikiana nao.

pamoja na hali hiyo anasema kuwa bado wamekuwa wakikabiliana na mbinu mbalimbali za majangili ikiwamo kutumia teknolojia mbalimbali kama kusaga meno au magamba ya tembo ili kutoyabaini kwenye mashine hasa kwenye viwanja vya ndege ambapo ndipo sehemu kubwa ambayo wamekuwa wakikamata meno ya tembo pindi wanapojaribu kuyasafirisha nje ya nchi.

“Kwa sasa sisi tawa tunaendelea na mkakati mbalimbali katika maeneo ambayo tuyasimamia na hakika tunaamini hatua hii tunakwenda nayo sambamba na kuimarisha teknolojia za kisasa katika maeneo yote muhimu kwa nchi yetu,” anasema Kanon

Naye Meneja ufuatiliaji mradi wa Tuhifadhi Maliasili unaofadhiliwa na USAID, John Noronha, amesema changamoto kubwa anayoiona ni kutotekelezwa kwa sheria na kanuni zinazoongoza uhifadhi na ulinzi wa wanyamapori.

“Migogoro tunayoiona kwenye hifadhi, amapori ya akiba na kwingineko tunaona baadhi ya viongozi hawasimamii kikamilifu utekelezaji wa sheria na kanuni zinazoongoza rasilimali, kutotenga na kupanga matumizi ya ardhi,” amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JETI, John Chikomo amesema ulinzi wa wanyama, uhifadhi wa maliasili unategemea zaidi ulimishaji jamii ndiyo maana wameamua kuwapa mafunzo wahariri ili waisambaze kwa urahisi elimu hiyo.

“Wahariri wakielewa na kutoa fursa kwa habari, Makala na vipindi kutangazwa jamii itaelewa, lengo letu ni kufanya mazingira, wanyama na maliasili ziendelee kuwapo na kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo,” amesema

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi waChama cha Waandishi wa Habari wa Mazingira Tanzania (JET), Bakari Kimwanga, akitoa maelezo kwa Wahariri kuhusu ufadhili wa mradi wa Tuhifadhi Maliasili unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here