Viongozi wa mapinduzi ya Niger wamempa balozi wa Ufaransa saa 48 kuondoka nchini humo huku uhusiano wa pande mbili ukiendelea kuzorota kwa kasi.
Junta ilisema Sylvain Itte amekataa kujibu mwaliko wa kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Niger.
Ufaransa, koloni ya zamani ya Niger, ilisema “wapuuzi hawana mamlaka” ya kuamuru kufukuzwa balozi huyo.
Paris inapinga mapinduzi ya Julai, ikisema kuwa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Bazoum lazima arejeshwe madarakani.
Tangazo hilo lasiku ya Ijumaa lilitolewa na waziri wa mambo ya nje wa Niger aliyepewa madaraka hayo na Junta
Hii inafuatia mfululizo wa kauli na maandamano dhidi ya Ufaransa.
Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilijibu kwa kusema kwamba “imezingatia hatua hiyo ya waasi”, shirika la habari la AFP liliripoti.
“Wapinzani hawana mamlaka ya kufanya ombi hili, idhini ya balozi inakuja tu kutoka kwa mamlaka halali zilizochaguliwa za Niger,” wizara iliongeza.
Chanzo: BBC