Raia wa Gabon wanapiga kura katika uchaguzi wa Rais, wabunge na serikali za mitaa. Katika uchaguzi huo, vyama vya upinzani vinashindana na Rais Ali Bongo vikitumai kupata ushindi na kukomesha utawala wa familia yake
Zoezi la uchaguzi nchini humo limeanza mapema leo asubuhi huku jumla ya wagombea 19 wakiwania nafasi ya Urais.
Hata hivyo Wagombea sita kati ya hao wanaotoka vyama vikuu vya upinzani wameungana na kumsimamisha mgombea mmoja.
Uchaguzi wa rais Gabon: Bongo kuchuana na wagombea 18
Uchaguzi unaofanyika leo Gabon unatarajiwa kuwa kipimo cha uungwaji mkono wa Rais Ali Bongo mwenye miaka 64, ambaye amekwisha kulitawala taifa hilo kwa kipindi cha miaka 14.
Rais huyo anatetea kiti chake katika muhula wa tatu.
Chanzo: DW