Home KITAIFA PSSSF YAELEZA MAFANIKIO YA MIAKA MITANO TANGU KUASISIWA KWAKE

PSSSF YAELEZA MAFANIKIO YA MIAKA MITANO TANGU KUASISIWA KWAKE

Google search engine

*YALIPA MADAI ILIYORITHI YA TRILIONI 1.03/-,IDADI YA WANACHAMA YAFIKIA 731,183, WATUMISHI VYETI FEKI WALIPWA BILIONI 35/-

*RAIS SAMIA SULUHU HASSAN APEWA SHUKRANI KWA MAGEUZI YA NDANI YA PSSSF

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba akizungumza wakati wa kikao kazi na Jukwaa la Wahariri kilichoandaliwa kwa pamoja kati ya Mfuko na Ofoso ya Msajili wa Hazina (TR) na kufanyika Makao Makuu ndogo ya PSSSF Jengo la Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam Agosti 31, 2023.
Mmoja ya Wahariri mkongwe, Joe Nakajumo akisoma kitini cha PSSSF

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Dk. Hosea Kashimba, amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa mfuko huo miaka mitano iliyopita wamefanikiwa kulipa madeni waliyoridhi kutoka kwenye mifuko mingine na kulipa madeni ya Sh Trilioni 1.03.

Pamoja na hilo pia amesema kwa kipindi cha miaka mitano kwenye ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wamefanikiwa kupata hati safi na kuufanya mfuko huo kuwa wenye mafanikio kwa jamii.

Akizungumza leo Agosti 31, 2023 kwenye mkutano na Wahariri wa vyombo vya Habari chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa lengo kueleza taarifa mbalimba za taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo na shughuli wanazofanya kwa umma.

Dk. Kashimba amesema wamepata mafanikio mbalimbali ambapo kiasi cha Sh Trilioni 1.03 kililipwa ndani ya miaka miwili kwa zaidi ya wanufaika 10,273.

“Thamani ya Mfuko imeongezeka kwa asilimia 27.76 kutoka Shilingi Trilioni 5.83 hadi Shilingi Trilioni 8.07. Zimepungua kutoka asilimia 12 hadi 5 ya michango inayokusanywa kwa mwaka ambapo kwa sasa Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wanalipwa kwa kanuni inayofanana

“Mfuko kwa sasa unalipa Fao la upotevu wa ajira ambapo mwanachama hulipwa asilimia 33 ya mshahara kwa muda wa miezi sita, Mfuko umeboresha huduma katika nyanja zote na kuwa na uwezo wa kutumia TEHAMA kwa asilimia 90 na pia tunalipwa kwa mujibu wa Mkataba wa ILO

“Mfuko ulianza na Mpango mkakati wa miaka mitatu, (2019/20- 2022/23), na sasa Mpango Mkakati wa Miaka mitano ((2022/23-2026/27) na pia umeendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ukifuata dira pamoja na dhima yake,” amesema Dk. Kashimba

“Pia tumelipa kiasi cha jumla ya Shilingu Trilioni 8.88 kwa wanufaika 262,095 na kuongeza thamani ya uwekezaji kwa asilimia 23.5, kutoka Shilingi Trilioni 6.40 hadi Shilingi Trilioni 7.92, wastani wa ongezeko la asimilia 4 kila mwaka

“Pia tunapata mapato yatokanayo na uwekezaji ya wastani wa asilimia 85 kwa mwaka ikiwamo kulinda na kuongeza thamani ya Mfuko kwa asilimia 27.76, kutoka Shilingi Trilioni 5.83 hadi Shilingi Trilioni 8.07, wastani wa ongezeko la 6.72 kwa mwaka,” amesema

Mkurugenzi huyo wa PSSSF, amesema kuwa wamefanikiwa kupunguza gharama za uendeshaji kutoka wastani wa asilimia 12 hadi 5 ya michango inayokusanywa kwa mwaka ikiwa ni chini ya ukomo wa asilimia 10 kwa mujibu wa taratibu na kanuni.

“Kulipa bila kukosa na kwa wakati, pensheni ya kila mwezi, wastani wa Shilingi bilioni 67 kwa wastaafu kila ifikapo tarehe 25 ya mwezi husika, hili ni ongezeko la asilimia 100 ukilinganisha na kiasi cha wastani wa Shilingi bilioni 34 wakati wa kuunganishwa

“Kupunguza muda wa kusubiri Mafao kwani Mfuko unalipa ndani ya siku 60, kwa mujibu wa sheria; kabla ya Mfuko wastaafu wengine walitumia zaidi ya miaka mitatu kusubiri Mafao. Kuboresha huduma za wateja kwa kutumia Mifumo ya TEHAMA iliyovumbuliwa, kutengenezwa na kuendeshwa na wataalamu wa ndani kwa asilimia 90.

“Kuwaunganisha Wafanyakazi wote waliotoka kwenye Mifuko minne iliyokuwa na tamaduni tofauti; na sasa wanalengo moja la kazi za Mfuko Mpya

“Kutenda kazi kulingana na Sheria, taratibu na miongozo ya Serikali; Ukaguzi wa Mahesabu na Manunuzi: Mfuko umepata hati safi za Hesabu za Mfuko toka uanzishwe na pia kupata tuzo za uandaaji na uwasilishaji bora wa Mahesabu kutoka NBAA kwa miaka miwili mfululizo 2020/21 na 2021/22,” amesema Dk. Kashimba

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba, (kulia) akisikiliza swali kutoka kwa Mhariri (hayupo pichani) na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Mkuti

MALIPO VYETI FEKI

Amesema baada ya ruhuma ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuagiza waliokutwa nav yeti feki walipwe haki zao, kupitia PSSSF tayari wamefanikiwa kulipa kiasi cha Shilingi Bilioni 35 hadi sasa.

MANUNUZI

Amesema kuwa katika kutekeleza kikamilifu taratibu za Manunuzi ya Umma Mwaka 2020/21 Mfuko ulishika namba moja kwa taasisi za Serikali kwa kupata matokeo ya asilimia 94 ya ukaguzi ya kuzingatiaji wa miongozo ya manunuzi ya Umma

“Pia tumefanikiwa kuandikisha Wanachama wapya 140,162 kwa wakati, hawa ni waajiriwa wa Serikali na taasisi zake pamoja na kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mifumo na miongozo ya ndani ya usimamizi wa rasilimali watu kwa kuzingatia utawala bora,” amesema

Amesema wanachama wao wengi wao ni waajiriwa wapya katika kada za Afya, Elimu, na Mashirika ya Umma na yale ambayo Serikali ina hisa zaidi ya asilimia 30 huku akitoa pongezi kwa Serikali kwa kuendelea kutoa ajira kwa Watanzania ambao ndio nguzo muhimu katika kuendeleza mfuko huo.

“Idadi ya wanachama kwenye Mfuko kwa sasa ni 731,183; ME ni 434,667 na KE 296,516,” amesema

Baadhi ya Wahariri walioshirki mkutano huo leo

UKUSANYAJI WA MICHANGO:

Amesema kiasi cha Shilinhi Trilioni 9.60 kimekusanywa, ambapo kiasi hicho kinajumuisha Shilingi trilioni 2.17 ambayo ni malipo  ya malimbikizo ya michango ya wanachama wa kabla ya Mwaka 1999 ya uliokuwa Mfuko wa PSPF

UWEKEZAJI

Dk. Kashimba, amesema kuwa thamani ya uwekezaji imeongezeka kwa asilimia 23.5; kutoka Sh Trilioni 6.40 hadi Trilioni 7.92, sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 4 kwa mwaka.

Ametaja kuwa uwekezaji huo umegawanyika katika masuala ya Hati fungani za Serikali asilimia 60, uwekezaji katika majengo asilimia 15 na kiwango cha upangishaji asilimia 100 kwa majengo ya makazi na asilimia 72 kwa majengo ya kupangisha kwa ajili ya ofisi ambapo  matarajio ni kufika asilimia 80 mwisho mwa mwaka wa fedha.

Mhariri Mtendaji wa Fama, Jesse Kwayu akulizwa swali kuhusu shughuli za Mfuko wa Hifadhi wa PSSSF leo

HUDUMA ZA WANACHAMA

Akizungumzia huduma kwa wanachama Dk. Kashimba, amesema kuwa mfuko huo unatumia TEHAMA kwa zaidi ya asilimia 90 katika kazi zake zote na inategemea kufika asilimia 100 ifikapo Juni, 2024.

“Mifumo hii ni matokeo ya uwekezaji na uvumbuzi wa Mfuko katika Mifumo kwa kutumia wataalamu wake ili kuboresha huduma kwa wateja na pia kuimarisha usalama katika kutunza nyaraka, kufanya malipo na kupokea malipo mbalimbali na matumizi  ikiwamo Waajiri kutengeza Ankara na kulipa michango ya  wanachama moja kwa moja bila kuhita msaada kutoka kwenye Mfuko.

“Wanachama kupata taarifa za uchangiaji wakati wowote kupitia mtandao bila kuhitajika kufika katika ofisi zetu. Wastaafu na wategemezi wanaweza kujihakiki kwa kutumia alama za vidole (biometric) bila kuhitaji kujaza fomu na kufika ofisini,” amesema

SHUKRANI KWA RAIS SAMIA

“Mafanikio ambayo Mfuko umeyapata kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

“Kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini wa Mfuko, namshukuru Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uthubutu wake wa kuamua kulipa deni la michango la shilingi trilioni 4.6 la Wanachama wa uliyokuwa Mfuko wa PSPF ya kabla ya Mwaka 1999, Uamuzi huu umewezesha Mfuko kulipwa kiasi cha Shilingi Trilioni 2.17 kupitia hatifungani maalum

“Serikalil pia imelipa shilingi bilioni 500 katika deni la shilingi bilioni 731.4 la Mikopo ya Miradi ambayo Mifuko iliyounganishwa iliikopesha Serikali ili kutekeleza Miradi ikiwemo ujenzi wa; Jengo la Bunge, Chuo Cha Serikali cha Hombolo, Nelson Mandela Istitute of Science and Technology na Chuo kikuu cha Dodoma. Huu wote ukiwa ni sehemu uwekezaji wa Mfuko.

“Jambo la kulipa madeni ya Serikali katika Mfuko, hususani lile la Michango ya kabla ya Mwaka 1999, lilichukua muda mrefu, takribani miaka 20. Hata hivyo, kupitia uongozi Madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Sita, jambo hili limewezekana,” amesema

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here