MWANDISHI WETU
-BEST MEDIA, ARUSHA
BENKI ya NMB imetoa misaada vifaa mbali mbali katika Hospitali ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha ikiwemo vitanda, magodoro, mashuka na makabati ikiwa ni njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya ambayo ni kiini cha maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Alfred Shao Amesema kuwa benki ya NMB ieendelea kutoa sehemu ya faida wanayoipata kuirudisha kwenye jamii kupitia misaada mbali mbali inayolenga kuboesha sekta za afya na elimu.
Alfred Amesema kuwa Benki hiyo imekua mstari wa mbele katika kusaidia jamii kwa kutambua kuwa wananchi ndio wanaifanya benki hiyo kuwa benki namba moja nchini Tanzania.
“Tunaipongeza serikali n tunaunga mkono juhudi hizo kwa kutoa misaada ya vifaa mbavyo tumevitoa ni pamoja na Vitanda 20 ,Mashuka 100,Makabati 20, Mabenchi 20 Vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni,” amesema Shao
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela ameishukuru benki ya NMB kwa kutoa misaada katika Wilaya zote za Mkoa wa Arusha na nchi nzima .
Mongela amewataka Watumishi wa afya kutoa huduma bora kwa wananchi kutokana na uboreshwaji wa huduma za afya unaofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo Benki ya NMB.
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Dadi Kolimba amesema kuwa wilaya hiyo imefaidika kwa kupata vifaa vya kutosha na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa NMB kwa kuendelea kuichangia hospitali hiyo lengo ni kuanza kutoa huduma Agosti mwaka huu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Dk. Lucian Mao mepongeza benki ya NMB kwa kutoa msaada huo ambao utasaidia hospitali ya wilaya kufanya kazi kwa ufanisi.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Karia Magaroa ameipongeza serikali na benki ya NMB kwa kutoa misaada inayogusa wananchi moja kwa moja.
Kwa upande wao wakazi wa Wilaya ya Karatu, wakiwemo wanawake Esta Dahay na Catherine Ibicha wamesema kuwa msaada huo utasaidia kuboresha afya ya mama na mtoto na kuwapunguzia wananchi adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.