*WADAI BIMA YA MAISHA WALIPWA MADENI YA BILIONI 63.21/-
Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
MKURUGENZI Mtendaji wa NIC Insurance, Dk.Elirehema Doriye amesema miaka 60 ya NIC Insurance ni mapinduzi makubwa yamefanyika katika kutoa huduma za bima nchini.
Hayo ameyasema leo Setemba 11, 2023katika mkutano ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina nchini na Wahariri wa vyombo vya Habari, ambapo amesema kuwa safari ya miaka 60 ilikuwa ya mabonde na milima lakini sasa mapinduzi yamefanyika katika NIC kutumia ubunifu kwenye mapinduzi ya teknolojia kwa kutengeneza mifumo ya Kidijitali ya kuwafikia kiurahisi na kufanya huduma zetu kuingia sokoni na kupokelewa kiurahisi.
Amesema katika mapinduzi ya Teknolojia NIC imeweza kupata Tunzo ya Superbrands Afrika Mashariki ambapo makapuni mengine hayajafikia tunzo hiyo.
“Mafanikio yetu yanatokana na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kufungua mipaka ya uwekezaji na biashara na kufanya NIC Insurance kupita katumia mipaka hiyo iliyofunguliwa na Rais Wetu,”amesema Dk.Doriye.
Amesema kuwa kasi yao haitaishia hapo kwani watanzania wanaitegemea NIC katika kuwafikia kutoa huduma za bima ili waweze kujenga uchumi ambao hata majanga yakitokea NIC kuwashika mkono kutokana na bima zao.
Hata hivyo amesema kuwa miaka 60 hiyo kwao ni sehemu ya deni kwa watanzania katika kuhakikisha wanawafikia katika makundi yote na kuwa NIC Insurance ni kimbilio la huduma bora za bima.
Aidha amesema kuwa NIC Insurance imekwenda mbali hadi kupata cheti cha kimataifa cha ISO kutokana na kutoa huduma bora kwa wateja
Amesema NIC Insurance inaendelea kuboresha huduma kwa viwango vya Kimataifa kwa sababu wanauzoefu katika bima wataendelea kuwa bora zaidi.
“Safari ya miaka 60 ilikuwa ya misusuko na changamoto mbalimbali ambazo ndizo zilizofanya kuwa bora katika utoaji wa huduma bora na imetupa hekima ya kuelezea watanzania wanataka nini na wanamuangalia mteja uwezo wa kumhudumia vizuri Ili twende na viwango vya Kimataifa kiwango kisicho pungua asilimia 90,”amesema Dk. Doriye
Amesema wanaendana na mabadiliko ya uchumi na Teknolojia katika utoaji bidhaa za bima zinazohutajika katika soko.
Aidha aesema bidhaa ambazo wanatengeneza kwenye bima za na bima za Maisha, Beam Life, Kilimo na nyinginezo kutokana na soko linavyokwenda katika mahitaji ya wananchi.
Kutokana na hali hiyo amesema kuwa NIC Insurance ni kampuni inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100, ikiwa na dhamana ya kufanya biashara ya bima za mali na ajali pamoja na bima za Maisha.
“Kati ya makampuni zaidi ya 30 yaliyopo kwenye soko la bima Tanzania, NIC insurance imeweza kumudu ushindani huu kwa kufanya vizuri baada ya maboresho mbalimbali yaliyofanyika tangu mwaka 2019,” amesema
UWEKEZAJI KATIKA MIFUMO YA TEHAMA
Kutokana na hali hiyo Dk. Doriye, amesema kuwa hatua ya uwekezaji katika Tehema kumeongeza mapato sambamba na kuondoa matumizi ya karatasi.
“kumepunguza muda wa kulipa madai hadi kufikia siku saba na kumerahisisha utoaji wa huduma. Bidhaa na huduma zetu zinapatikana Kidijitali kwa mfano asilimia 13 ya mapato yetu ya bima yameandikishwa kidijitali,” amesema
MAPATO KWA KIPINDI CHA (2019/20-2021/22)
Akizungumzia mapato Dk. Doriye, amesema kuwa kutokana na kuchukua hatua kadhaa NIC imeweza kuondoa hasara kwa kuongeza mapato kutoka Sh bilioni 76.45 kwa mwaka wa fedha 2019/20 hadi Sh bilioni 103.94 kwa mwaka 2021/22 ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 17.98 kwa mwaka.
Amesema hatua ya uwepo wa usimamizi madhubuti wa matumizi pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi kumeongeza ufanisi na kuondoa matumizi yasiyo na tija jambo lililoshusha gharama za uendeshaji na kuongeza faida.
“Katika kipindi cha miaka mitatu tumelipa madai ya bima za wateja ambapo hadi kufikia Juni 2022, tumelipa jumla ya Shilingi bilioni 33.79 kwa bima za Maisha na Shilingi bilioni 40.18 kwa bima za mali na ajali.
“Tumeweza kulipa kodi ya mapato Serikalini kutokana na faida inayopatinana ambapo ulipaji huo umeongezeka kutoka Shilingi billioni 11.86 mwaka 2019/20 hadi Shilingi bilioni 15.14 mwaka 2021/22 sawa na wastani wa asilimia 13.80 kwa mwaka.
“Faida ghafi imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 33.65 mwaka 2019/20 hadi Shilingi bilioni 63.21 mwaka 2021/22 sawa na asilimia 43.91 kwa mwaka,” amesema Dk. Doriye
MALI ZA NIC INSURANCE
Akieleza kuhusu mali amesema kuwa zimekua kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, kutoka mali zenye thamani ya Shilingi bilioni 350.36 mwaka 2019/20 hadi kufikia mali zenye thamani ya Sh bilioni 423.99 mwaka 2022.
“Ukuaji huu ni sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 10.51 kwa mwaka. malimbikizo ya faida ya Shilingi bilioni 45.74 kufikia Juni, 2022 kutoka kiasi cha malimbikizo ya hasara ya shilingi bilioni 19.31,” amesema
UKUAJI WA MTAJI WA WANAHISA
Amesema ufanisi katika uendeshaji, umewezesha ukuaji wa Mtaji wa wanahisa kuongezeka kutoka Sh bilioni 72.16 mwaka 2019/20 hadi Sh bilioni 217.07 mwaka 2021/22, ambapo ukuaji huu wa mtaji ni sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 100.40 kwa mwaka.
UKUAJI WA UWEKEZAJI KATIKA AMANA ZA BENKI
Dk. Doriye amesema kuwa uwekezaji katika hati fungani za Serikali kwa mwaka 2021/22 umefikia kiasi cha Sh bilioni 105.64 uKIlinganisha na kiasi cha Sh bilioni 51.58 kilichokuwepo mwaka 2019/20.
“Ongezeko hili ni sawa na wastani wa asilimia 52.40 kwa mwaka. Uwekezaji katika amana za Benki mwaka 2021/22 umefikia kiasi cha Shilingi bilioni 32.23 ukilinganisha na Shilingi bilioni 19.53 kilichokuwepo mwaka 2019/20. Ongezeko hili la uwekezaji kwenye amana za Benki ni sawa na wastani wa asilimia 32.54 kwa mwaka,” amesema
UTOAJI WA GAWIO
Amesema kuwa kwa mwaka ulioishia Juni, 2022 tumetoa gawio la Sh bilioni 2.0 kwa Serikali ikilinganishwa na gawio la kiasi cha Sh bilioni 1.5 lililotolewa mwaka ulioishia Juni 2021.
ONGEZEKO LA MTAJI
Kutokana na hali hiyo Dk. Doriye, amesema kuwa katika kukabiliana na uwezo mdogo wa kuhimili hasara inayoweza kutokea wamefanikiwa kuongeza mtaji wa kiasi cha Sh bilioni 12.05 kwa Aprili, 2022 sawa na ongezeko la asilimia 408.47 kutoka mtaji uliokuwepo wa kiasi cha Sh bilioni 2.95 na kufikia mtaji wa kiasi cha Sh bilioni 15 kilichopo sasa.