Home KITAIFA DK. JAFO AWATAKA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA AJENDA YA USAFI NCHINI

DK. JAFO AWATAKA WAKUU WA MIKOA KUSIMAMIA AJENDA YA USAFI NCHINI

Google search engine
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk. Selemani Jafo, akizungumza na wafanyabishara wa Soko la Machinga Jijini Dodoma leo Septemba 15, 2023 kuhusu kampeni ya usafi ya kila mwezi nchini

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk. Selemani Jafo amewahimiza wakuu wa mikoa kusimamia ajenda ya usafi wa mazingira kila Jumamosi asubuhi ili kuifanya miji kuwa safi.

Pia, ameelekeza kila mwananchi ashiriki kikamilifu kufanya usafi katika eneo linalozunguka nyumba yake ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Dk. Jafo ametoa kauli hiyo, leo Septemba 15, 2023 wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kuongoza zoezi la usafi wa mazingira kuadhimisha Siku ya Usafi Duniani katika Soko la Machinga jijini Dodoma.

Amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa zinasimamia kikamilifu usafi wa mazingira katika masoko yaliyopo katika maeneo yao unakuwa wa kudumu.

Waziri Jafo amewaelekeza watendaji wa mamlaka hizo kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa taka na kutupwa kwenye madampo yaliyopo katika maeneo yao bila kuzagaa ovyo.

“Kama mnavofahamu hapa nchini tunazalishaji takriban tani saba za taka lakini tani chache tu ndio zinatupwa dampo. Tunaadhimisha siku hii ya usafi kwa lengo la kuhakikisha mazingira ya Tanzania yanakuwa safi na ndio maana tumeelekeza majiji na manispaa wanakuwa na mikakati ya kutenga bajeti kuhakikisha taka zinasombwa kila mara ili zisirundikane,” amesisitiza

Aidha, Dk. Jafo ameupongeza uongozi wa Jiji la Dodoma kwa kusimamia vyema usafi wa mazingira kwa kuwa navitendea kazi vikiwemo magari na kutaka mamlaka zingine ziige mfano huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amnesema kuwa maelekezo ya Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu Bonde la Mzakwe jijini humo yamefanyiwa kazi.

Amesema kuwa miti iliyopandwa imeanza kukua pamoja na miumdombimu ya kuzuia moto na operesheni kuwachukulia hatua wavamizi zinaendelea ili kuhakikisha eneo hilo linarudi katika uoto wa asili.

“Mheshimiwa Waziri sasa hivi tumeanza kukamata wanaoingiza mifugo na wanaochoma mkaa kwenye Bonde la Mzakwe na yote haya ni maelekezo ya Serikali kuhakikisha chanzo hicho cha maji kinatunzwa,” amesema.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here