Na MWANDISHI WETU
-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kuwa wakati Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TMDA) ikitimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, amewataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kuunga mkono mageuzi makubwa yanayofanywa na taasisi hiyo.
Kutokana na hali hiyo amesema kuwa ni lazima jamii isaidiwe kwa kueleza mambo muhimu yanayofanywa na taasisi hiyo ikiwamo suala la uchnguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwani masuala hayo yanagusa maisha ya watu kila siku.
Hayo ameyasema leo Septemba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifungua kikao kazi kati ya TMDA na wahariri wa vyombo vya Habari, ambapo amesema kuwa ni vema kuwa na ushirikiano wa pamoja ambao utasaidia kupata taarifa sahihikatika utekelezaji wa majukumu utawezesha upatikanaji wa taarifa sahihi ambazo zitakuwa msaada kwa jamii.
RC Chalamila, amesema kuwa vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kufikisha taarifa Kwa jamii jambo ambalo ni vema kuwa na mahusiano mema katika ya yao (wahariri)na TMDA.
Awali akizungumza katika kikao kazi hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo amesema kuwa katika kipindi cha miongo miwili katika usimamizi wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kusimamia na kufanya uchunguzi katika eneo hilo kama njia ya kuhakikisha dawa na vifaa vyombo vinavyotumika vinakuwa na ubora unaotakiwa kwa mujibu wa sheria.
“Jambo kubwa ambalo sisi kama mamlaka tunalosimamia ni kuhakikisha jamii ya Watanzania wanalindwa kwa kuwa na vifaa tiba pamoja na kuwa na matumizi sahihi ya dawa.
Akieleza mafanikio yaliyopatika kwa mwaka 2011 maabara ya TMDA imetambuliwa kuwa mahiri ambapo ilimbuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO Prequlified Laboratory), 2012 kuwa Kituo cha umahiri wa usajili dawa barani Afrika na 2013 kuwa maabara ya mafunzo ya umahiri kwa Mamlaka za Udhibiti Dawa barani Afrika.
Fimbo, ameyataja mafanikio mengine kuwa ambapo mwaka 2014 walianzisha mifumo ya kielekroniki ya utoaji huduma Kwa wateja, 2015 Kutoa huduma za udhibiti kwa njia ya kielektroniki na kuimarika kwa makusanyo hivyo kuchangia asilimia 15ya mapato yake katika gawio la Serikali na kuwa na ziada ya asilimia 70.
“Mwaka 2017 tumefanikiwa kuanzisha mazingira wezeshi na rafiki ya ufanyaji biashara nchini kwa bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA, 2018 Kufikia Ngazi ya tatu ya Shirika la Afya Duniani – WHO (WHO Maturity L-3) kwa kuwa na mifumo bora ya udhibiti dawa barani Afrika.
“… hivyo kuwa taasisi ya kwanza ya udhibiti na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia ngazi hiyo na kupata hadhi ya juu ya ngazi ya nne umahiri wa Shirika la Afya Duniani (Quality Control LAB WHO ML 4),” amesema Fimbo
Mwisho