Home KITAIFA PPRA YABAINI MAZITO MFUMO TANePS, SASA KUWASHA NeST

PPRA YABAINI MAZITO MFUMO TANePS, SASA KUWASHA NeST

Google search engine

*MANUNUZI YOTE YA SERIKALI KUDHIBITIWA KWENYE MFUMO MMOJA KUONDOA RUSHWA, USALAMA WA NCHI SASA KUWA IMARA

* TANePS KUZIMWA SEPTEMBA 30, 2023, WATANZANIA WATAKIWA KUJISAJILI KWENYE MFUMO MPYA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Eliakim Maswi akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani) leo Septemba 22, 2023, kuhusu manufaa ya kuanza kutumia kwa mfumo mpya wa manunuzi ya Serikali wa NeST
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Eliakim Maswi akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani) leo Septemba 22, 2023. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile
Wahariri walioshiriki mkutano huo, akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Eliakim Maswi (hayupo pichani)
Mhariri Mtendaji wa Media Brain, Jesse Kwayu ( kushoto) akiwa na Mhariri Mkuu wa Gazeti la Rais Mwema, Joseph Kulangwa (katikati) pamoja na Mhariri kutoka Uhuru FM ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF, Angellah Akilimali , akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Eliakim Maswi (hayupo pichani)

Na MWANDISHI WETU

-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeanzisha mfumo mpya wa manunuzi wa kielekroniki National e-Procurement System of Tanzania (NeST) na kulazimika kuachana na ule wa awali ambao hakuwa salama kwa usalama wa nchi.

Hatua hiyo inatokana na mfumo huo kuendeshwa na Kampuni kutoka nchini Ugiriki inajulikana kwa jina la European Dynamics ambapo kwa mujibu wa mkataba kampuni hiyo ndiyo mmiliki wa mfumo na mwendeshaji wa mfumo huo.

Kutokana na hali hiyo imeelezwa kwamba mkataba wa uendeshaji na usimamizi wa mfumo huo sasa unafikia ukomo Desemba 31, 2023.

Akizungumza leo Sepemba 22, 2023 na Wahariri wa Vyombo vya habari nchini, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Eliakim Maswi, amesema kuwa baada ya Serikali kufanya tathmini ya kina ya mfumouliopo wa TANePS wataalamu walishauri kujengwa kwa mfumo mpya ajili ya kupata ufumbuzi wa changamoto za mfumo ulipo sasa kukidhi mahitaji ya Serikali.

“Mfumo wa NeST utakuwa na uwezo wa kuongeza uwazi na uwajibikaji, utakidhi mahitaji ya sheria za nchi, taratibu na miongozi ya ununuzi. Lakini pia kuwa na mfumo wa NeST unakwenda kupunguza mianya ya rushwa na kuleta thamani halisi ya fedha za Serikali katika ununuzi wa umma.

“Lakini pia utakuwa mfumoutakaokuwa rahisi katika kutumia na kuongeza wigo kwa watumiaji. Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Serikali Mtandao (eGA) iliamua kufanya tathmini,  ambapo Februari 2022 ilionekana wazi kwamba mfumouliopo hauwezi kukidhi mahitaji ya sasaya Serikali ni vigumu kuweza kupata ufumbuzi wa changamoto zilizopo na uendeshaji wa mfumo, ambapo sasa hata sisi PPRA tukitaka jambo lazima tuwasiliane na mwendeshaji ambaye yupo Ugiriki.

“…timu ya wataalamu iliishauri Serikali ianze kazi ya kujenga mfumo mpya pamoja na mambo mengine kutatua changamoto zilizopo kwenye mfumo uliopo. Serikali ilipomtaka mzabuni aweze kuwezesha Serikali kuwa na Full control ikiwemo kuwa na Full Source Code, mzabuni aliiambia Serikali italazimika kulipa Dola za Marekani milioni 25 (zaidi ya Shilingi bilioni 65),” amesema Maswi

Kutokana na hali hiyo Maswi, amesema kuwa iwamo Serikali ingelea kurithi matatizo yaliyopo kwa sasa ya kuwa na mfumo ambao haukidhi mahitaji ya watumiaji na kama itataka mfumo huo uhuishwe, Serikali italipa gharama kubwa.

“Uwezekano wa gharama za kuhudumia kuwa kubwa kutokana na mkandarasi kutokuwa na ushindani. Iwapo Serikali itaamua iisingie mkataba mpya na mkandarasi na kuamua kutumia mfumo ulivyo, changamoto itakuwa kubwa wakati wa matumizi kwani wataalamu wa Tanzania hawana ujuzi wa kuhudumia mfumo ambao pia hata kwa usalama wa nchi ni hatari,” amesema

Ofisa Mtendaji Mkuu huyo wa PPRA, amesema kuwa changamoto nyingineni mkataba wa mkandasi wa kuhudumia mfumo unaisha Desemba 31,2023 na iwapo Serikali isingeweza kuwa na mfumo mbadala wakati huu yapo masuala kadhaa yangejitokeza ikiwamo muda wa vifaa utakuwa umemalizika na Kampuni ya European Dynamics ingeitaka Serikali inunue vifaa vingine kulingana na matakwa yao wenyewe na sio mahitaji ya Serikali.

YALIYOBAINIKA

Maswi, amesema kuwa hadi kufikia Juni 2023 taasisi nunuzi 864 zimesajiliwa kwenye mfumo na ndio zilizopaswa kutumia mfumo huoambapo wazabuni 37, 445 wamesajiliwa kwa ajili ya kutumia mfumo.

Amesema tangu kuanza kutumia mfumo zaibuni 142,606 zilitangazwa kwa kutumia mfumo wa zabuni zilizoendela hadi kupata tuzo (awarded) kwa kutumia mfumo ni 26,366 sawa na asilimia 18.5 na hivyo kuonesha kiwango kidogo katika kukamilisha mchakato wa ununuzi kwa kutumia mfumo huo.

“Kati ya zabuni zilizotangazwa zaidi ya asilimia 81.5 ya zabuni hizo hazikumaliza mchakato wake kwa kutumia mfumo. Wakati mfumo wa sasa wa NeST ni rahisi na unatumia dakika 30 na umeunganishwa na Brela ikiwamo taasisi zote nasi PPRA ataweza kuona kila kitu kwa wakati huohuo jambo ambalo litaleta ushindani wa kweli na wa haki.

“Tunajua wapo waliokuwa wakiomba zabuni maana halisi ya zabuni kuomba mtandaoni ni kupunguza na kuondoa kabisa rushwa lakini kupitia mfumo huu mpya mengi tunayaona kwa wakati na hata kuweza kuwasiliana na wahusika kama kuna jambo ambalo haliko sawa,” amesema Maswi.

Amesema mfumo wa NeST utasaidia kudhibiti rushwa, mchakato wa zabuni kuchelewa na kuongeza uwazi wa zabuni.

Mfumo huo uliobuniwa na kutengenezwa na watanzania wenyewe umeanza kufanya kazi Julai 1, mwaka huu ukichukua nafasi ya mfumo wa awali wa TANePS utakaokoma kufanya kazi itakapofika Septemba 30, mwaka huu.

Maswi amewataka wafanyabiashara wote kuomba zabuni kwa kutumia mfumo huo mpya kama wanataka kupata kazi za serikali.

Alisema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amedhamiria kubadilisha utendaji wa mamlaka hiyo na anataka itoke mahali ilipo kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo matumizi ya mifumo ya kielektroniki kuleta tija na ufanisi unaostahili.

Amesema taasisi zinazosimiwa na Msajili wa Hazina na Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (TAMISEMI), zinapaswa kuanza kutumia mfumo mpya kwa shughuli za ununuzi wa umma na kwamba itakapofika Oktoba Mosi mwaka huu taasisi nunuzi zote za serikali hazitaweza kutuma mialiko ya zabuni katika mfumo wa zamani wa TANePS.

Hivi karibuni Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha sheria mpya ya manunuzi kwa lengo la kuleta ufanisi na uwazi katika manunuzi ya umma

Hata hivyo inaelezwa kwmaba asilimia 70 ya bajeti ya serikali inatumika kwenye ununuzi kwa hiyo panapokuwepo na sheria na mifumo mizuri fedha za serikali zinatunusurika.

WATANZANIA WASISITIZWA

Kutokana na hali hiyo Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imewasisitizia watu waliopo kwenye makundi maalum ambayo ni vijana, wazee, wanawake na watu wenye ulemavu kujisajili kwenye Mfumo Mpya wa Ununuzi kwa njia ya Mtandao (NeST) ili kunufaika na upendeleo uliopo katika fursa za ugawaji wa Zabuni za umma nchini.

Afisa Mtendaji Mkuu huyo wa PPRA, amesema kuwa Mfumo wa NeST unawatambua na kuwazingatia wazabuni waliopo kwenye makundi hayo.

“Mfumo unawatambua watu wa makundi maalumu, kwa hiyo wanachotakiwa kufanya ni kufuata taratibu za kurasmisha vikundi vyao katika ngazi za halmashauri kisha wajisajili kwenye mfumo wa NeST,” amesema Maswi

Aidha amesema kuwa Katika Mfumo wa TANePS usajili wa makundi maalumu haukuwa mkubwa, hivyo amewasihi wenye sifa za kuwa makundi maalum na wanahitaji kushiriki zabuni za umma kujisajili katika mfumo wa NeST ambao ni rafiki zaidi kwa watumiaji wote.

“Serikali yetu inawajali watu wote na inataka kila mtanzania mwenye sifa aweze kushiriki zabuni za umma na kujiinua kiuchumi, sio tu kwa makampuni hata watu binafsi waliosajiliwa pamoja na watu ambao wako katika uchumi wa chini ambao wanaweza kushiriki kupitia fursa ya makundi maalum hata bila kuwa makampuni,” amesema.

Maswi, amesisitiza kwamba zipo kazi nyingi ambazo kwa mujibu wa sheria zimetengwa kwa ajili ya makundi maalumu na kwamba mfumo wa NeST utaongeza kwa kiasi kikubwa ushiriki wa wazabuni kwa kuwa unaongeza uwazi, ushindani na kuondoa urasimu usio na sababu za msingi.

FURSA ZA WAZABUNI

Fursa za ugawaji wa zabuni kwa makundi maalumu zinasimamiwa na kushughuliwa kwa kuzingatia vifungu vya Sheria ya ununuzi ya Umma sura 410 inayozitaka taasisi zote za umma nchini kutenga asilimia 30 ya bajeti ya Ununuzi kwa mwaka kwa ajili ya makundi maalumu.

Kwa mujibu wa Mwongozo wa Makundi Maalumu uliotolewa na PPRA mwaka 2020, makundi maalumu yamegawiwa asilimia 10 kwa vijana, asilimia 10 kwa watu wenye ulemavu, asilimia tano kwa wanawake na asilimia tano kwa ajili ya wazee.

Maswi amesema kuwa PPRA bado inaendelea kutoa mafunzo wezeshi ya matumizi ya Mfumo wa NeST kwa Wazabuni na Taasisi nunuzi kote nchini ili kuhakikisha kuwa umma wa watanzania wanajengewa uwezo na kuchangamkia fursa katika ununuzi wa umma nchini.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here