-KILA KITONGOJI NCHINI KUFUNGANISHWA UMEME
ZUENA MSUYA NA THERESIA LUGWISHA
-TABORA
NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema kuwa ifikapo Desemba mwaka huu, utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko wa Pili katika vijiji vyote utakamilika na hivyo kupelekea kuanza utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme vitongojini.
Hayo ameyaseme katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo katika Mkoa wa Tabora ambapo katika siku ya pili ya ziara yake amewasha umeme katika kijiji cha Katunda wilayani Uyui mkoani humo.
“Tunatarajia kumaliza kazi ya kusambaza umeme vijijini ifikapo mwezi Desemba mwaka huu, nawahimiza wakandarasi fanyeni kazi yenu kwa uadilifu mkubwa, hatuhitaji kukimbizana juu ya hilo kila mmoja atekeleze jukumu lake kwa maslahi mapana ya taifa letu,” amesema Kapinga.
Kutokana na hali hiyo, amewaagiza wakandarasi wote nchini kuhakikisha kuwa vifaa vya kufanyia kazi vinakuwepo wakati wote katika maeneo ya miradi ili kurahisisha utekelezaji wa mradi huo na hivyo kuukamilisha kwa wakati.
Pia, amewataka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kukagua vifaa vya wakandarasi ili kujihakikishia kama vipo vyote katika karakana zao ili kuhakikisha kuwa kazi zinafanyika kwa wakati na zinaendana na muda wa mkataba uliowekwa.
Vilevile, amewataka REA kuchukua hatua stahiki kwa wakandarasi wote watakaokwenda kinyume na makubaliano ya mikataba ya kupeleka umeme vijijini.
Kapinga amewaagiza REA kuendelea kuwasimamia wakandarasi kwa karibu kwakuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha fedha inazozitoa zinaenda kuwafikishia wananchi umeme kama alivyoelekeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Naibu Waziri wa Nishati amewasisitiza wananchi kuendelea kusuka nyaya katika nyumba zao ili kujiweka tayari kuunganishiwa umeme pindi utakapowafikia katika maeneo yao na kwamba watu wote watafikiwa na umeme.
Akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Tabora na kuwaeleza kuwa watanzania wanataka umeme hivyo wafanye kazi kwa weledi, juhudi na maarifa usiku na mchana kuhakikisha watanzania wote wanapata umeme na kuwatatulia changamoto za umeme zinazowakabili wananchi hao.
I’ve been surfing online more than 3 hours today, but I never found any fascinating article like yours. It is lovely worth sufficient for me. Personally, if all site owners and bloggers made good content as you did, the internet will likely be a lot more helpful than ever before.
Thank you for continuing to collaborate and consult and do not stop visiting our Bestmedia network