Home KITAIFA WALIOPISHA MRADI WA UMEME UHURU KULIPWA FIDIA OKTOBA MWAKA HUU

WALIOPISHA MRADI WA UMEME UHURU KULIPWA FIDIA OKTOBA MWAKA HUU

Google search engine
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga (Katikati)akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Sospeter Oralo (aliyenyoosha mkono) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Uhuru wilayani Urambo Mkoani Tabora alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa kituo hicho, tarehe 27 Septemba, 2023.
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga(wa pili kulia) na mkuu wa wilaya ya Urambo, Kenan Kihongosi(kulia) wakikagua Maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Kupoza na kusambaza umeme cha Uhuru wilayani Urambo Mkoani Tabora wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa kituo hicho, tarehe 27 Septemba, 2023.
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga(Kulia)akifurahi na baadhi ya wanafunzi wa moja ya shule za msingi katika kijiji cha Mtakuja wilayani Urambo Mkoani Tabora waliofika kumlaki alipokenda kuwasha umeme katika kijiji hicho na kuzungumza na wananchi wakati wa ziara yake wilayani humo tarehe 27 Septemba, 2023.
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga(kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Kenani Kihongosi(kushoto) wakiteta jambo katika Kijiji cha Mtakuja wilayani humo Mkoani Tabora walipofika kuwasha umeme katika kijiji hicho na kuzungumza na wananchi wakati wa ziara yake tarehe 27 Septemba, 2023.
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga(katikati),Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Kenan Kihongosi( wa Nne kushoto) na Mbunge wa jimbo la urambo, mama Magreth Sitta(wa tatu kulia) wakikata utepe ili kuwasha umeme na Kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Mtakuja wilayani Urambo Mkoani Tabora wakati wa ziara wilayani humo tarehe 27 Septemba, 2023.

ZUENA MSUYA NA THERESIA LUGWISHA

-TABORA

SERIKALI imesema itaanza kuwalipa fidia ya Sh milioni 399 kwa wananchi 496 waliopisha Mradi wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Uhuru kilichopo katika Kijiji cha Vumilia Wilayani Urambo mkoani Tabora.

Hayo yamesemwa Septemba 27, 2023 na Naibu Waziri wa Nishati, katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kilichopo wilayani Urambo.

Amesema fedha hizo za fidia zitaanza kulipwa kuanzia mwanzoni mwa Oktoba ambapo taratibu zote za ulipaji fidia hiyo zimekamilika.

“Wananchi nawaomba muandae nyaraka zote muhimu  zikiwepo barua na vitambulisho vinavyothibitisha kulipwa fidia ili tarehe 2 Octoba, 2023 mtakapoanza kulipwa fedha zenu kusitokee changamoto ya aina yeyote itakayochelewesha malipo hayo, fedha ziko tayari na taratibu zote zimekamilika,” amesema Kapinga.

Aidha amesema ujenzi wa mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 66 ya utekelezaji wake unaendelea vizuri.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutaimarisha huduma ya upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi na mikoa mingine iliyo jirani.

Mradi huyo pia unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Kigoma pamoja na vituo viwili vya kupoza na kusambaza  umeme vya Urambo na  Nguruka.

Vilevile mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Katavi, pamoja na ujenzi wa vituo vitatu vya kupoza na Kusambaza Umeme vya Ipole, Inyonga na Mpanda.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kapinga, amewasha umeme katika Kijiji cha Mtakuja wilayani Urambo pamoja na kuzungumza na Wananchi.

Amewasihi wananchi kulinda na kutunza miundombinu ya umeme kwa kuwa Serikali imetoa fedha nyingi kutekeleza mradi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Kenani Kihongosi ameishukuru Serikali kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha upatikaji wa huduma za kijamii ikiwepo, umeme, vituo vya afya, maji, shule na barabara katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Ziara hiyo imehudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Urambo, Margareth Sitta, viongozi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini(REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Naibu amefanya ziara ya siku tatu ya kukagua maendeleo ya mradi wa usambazaji wa umeme vijijini awamu ya Tatu Awamu ya Pili katika Wilaya za Nzega, Uyui na Urambo kwa kuwasha umeme katika baadhi vijiji na kuzungumza na wananchi.

Google search engine

2 COMMENTS

  1. Does your website have a contact page? I’m having a tough time locating it but, I’d like to shoot you an e-mail. I’ve got some recommendations for your blog you might be interested in hearing. Either way, great blog and I look forward to seeing it develop over time.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here