Home KITAIFA TASAC YAELEZA FURSA ZILIZOPO SEKTA USAFIRISHAJI KWENYE BAHARI, MAZIWA

TASAC YAELEZA FURSA ZILIZOPO SEKTA USAFIRISHAJI KWENYE BAHARI, MAZIWA

Google search engine

*WAFANIKIWA KUFANYA UKAGUZI WA MELI ZA KIMATAIFA ZAIDI YA 200, IDADI YA VYOMBO VIDOGO ZAIDI KUONGEZEKA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nelson Mlali, akitoa taarifa kuhusu majukumu na mafanikio ya Shirika hilo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nelson Mlali, akiwa na viongozi wengine wa shirika hilo ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kukutana na Wahariri na Waandishi wa habari,  kilichofanyika Oktoba 5,2023 Jijini Dar es Salaam. (kulia) ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Mkuti.

Na MWANDISHI WETU

DAR ES SALAAM

KAIMU Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nelson Mlali amesema, kuna fursa nyingi katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji.

Kauli hiyo ameitoa Oktoba 5, 2023 Jijini Dar es Salaam katika semina ya Wahariri wa vyombo vya habari iliyoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, ambapo Mlali, ametaja miongoni mwa fursa hizo kuwa ni pamoja na kuanzisha usajili wa meli kwa masharti rafiki, uanzishwaji wa maeneo ya ukarabati na ujenzi wa meli katika Ukanda wa Pwani.

Pia uanzishwaji wa maegesho ya boti ndogo katika Ukanda wa Pwani, uanzishwaji wa viwanda vya utengenezaji malighafi za ujenzi wa boti za plastiki, ujenzi wa bandari rasmi za uvuvi zenye tija kwa nchi na nchi jirani ili kukuza mapato.

“Kuongezeka kwa idadi ya leseni za vyombo vidogo ambapo hadi sasa vimefikia 6,366 huku kazi ya kuongezeka kwa idadi ya vyeti kwa mabaharia waliokidhi masharti ambao wamefikia 17, 689 ambao wanafanyakazi nchini na wengine Serikali imewapelaka nje ya nchi kwa ajili ya kusomea kazi ya ukaguzi wa meli za kimataifa,” amesema Mlali

Amesema, utendaji kazi kwa umakini wa hali ya juu wa shirika hilo, umewezesha kupata hati safi mfululizo kuanzia mwaka 2018 hadi 2021.

Amesema TASAC ilianzishwa chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura ya 415 na kuanza rasmi kutekeleza majukumu yake Februari 23, 2018 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 53 lilitolewa Februari 16, 2018.

“TASAC ilianzishwa ili kuweza kutekeleza majukumu ya kusimamia usafiri kwa njia ya maji, usalama, ulinzi na udhibiti wa mazingira ya Bahari dhidi ya uchafuzi utokanao na shughuli za meli, jukumu ambalo lilikuwa likitekelezwa na SUMATRA,” amesema

Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura ya 415, majukumu makuu ya TASAC yapo kwenye vifungu Na. 7, 11 na 12 ikiwamo kufanya kazi za Uwakala wa Forodha (Clearing & Forwarding Function) kwa bidhaa chache zenye maslahi mapana kwa Taifa. Kazi hizo ni pamoja na ugomboaji na uondoshaji wa

Katika kuhakikisha wanasimamia majukumu ya TASAC pia ina wajibu wa kuhakikisha inasimamia kazi za Bandari hasxa kwenye ukaguzi wa Silaha za Moto na vilipuzi, Makinikia, Kemikali zinazoagizwa na kutumika na kampuni za uchimbaji madini, Nyara za Serikali na Wanyama hai kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa Wanyamapori.

“Katika jukumu la uwakala wa forodha, Shirika linafanya yafuatayo kuhakiki nyaraka za wateja za uingizaji na uondoshaji shehena, kuratibu ufuatiliaji wa vibali kutoka mamlaka mbalimbali, kuandaa kadhia kupitia mifumo ya forodha na kufuatilia malipo ya kodi.

“kufuatilia nyaraka za usafiri na usafirishaji kutoka kwa wakala wa meli, kushiriki katika ukaguzi wa shehena kwenye maeneo ya kiforodha, kuratibu na kufuatilia ankara za malipo ya gharama za bandari, kuratibu usafirishaji wa shehena, kutoa ushauri kwa waagizaji na wasafirishaji wa shehena kuhusu taratibu za kiforodha kwa shehena zilizoainishwa, zinapoingia au kutoka nchini,” amesema Mlali

KADHIA 10,000 ZASHUGHULIKIWA

Pia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limefanikiwa kuongeza idadi ya kadhia zilizohudumiwa kutoka kadhia 6,000 mwaka 2019/2020 hadi kufikia kadhia 10,000 mwaka jana.

TASAC pia imeunda nyenzo za udhibiti wa usafiri majini ikiwa ni pamoja na Kanuni na Miongozo ili kuwezesha utekelezaji wa sheria katika kudhibiti usafiri majini.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa TASAC alitumia semina hiyo, imeelezea mafanikio iliyoyapata hasa kutokana na usikivu wa Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kupokea ushauri wa kitaalam na kutoa maelekezo sahihi kupitia Wizara ya Uchukuzi, na kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali pamoja na kamati za Bunge.

Aidha, wamefanikiwa kuongeza idadi ya watoa huduma wanaodhibitiwa na TASAC, kwa maana ya idadi ya leseni na vyeti vya usajili vilivyotolewa,pamoja na  kuongezeka kwa idadi ya vyeti kwa mabaharia waliokidhi masharti.

Kutokana na hali hiyo, Mlali amesema wamefanikiwa kuimarisha udhibiti wa huduma za bandari baada ya urasimishaji wa maeneo 20 ya kibandari katika mwambao wa bahari na maziwa.

MIKATABA YA KIMATAIFA NA TUZO

Mlali amesema wamefanikiwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa mikataba, itifaki na miongozo inayotolewa na Shirika la Bahari Duniani (IMO) nakuridhiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Utekelezaji wa Mikataba ya Kimataifa kuhusu, Usafirishaji Majini inayoratibiwa na Shirika la Bahari Duniani (International Maritime Organization – IMO), Kufanya ukaguzi wa meli zilizosajiliwa nchini na meli za nje zinazoingia katika bandari za Tanzania Bara, Kudhibiti vivuko (Ferries),” amesema

Mbali na hayo, amesema kupata tuzo ya mshindi wa kwanza kitaifa na Kupata cheti cha ubora cha mfumo wa usimamizi wa ubora.

BOTI ZA UOKOZI

Katika hatua nyingine, Mlali amesema kuwa Shirika hilo linaendelea na utekelezaji wa ujezi wa boti tano za uokozi ambapo mbili zitakuwa ziwa Victoria, mbili Ziwa Tanganyika na moja Ziwa Nyasa.

“Tunatekeleza ujenzi wa boti tano za uokozi ambapo tunataka tuweke pale ziwa Victoria boti mbili, ziwa Tanganyika mbili na pale ziwa Nyasa boti moja, taratibu zimeshaanza kuangalia uwezekano wa kufanya vitu hivyo ili baadae tufike mahala tuweze kuwa na boti hizo za uokozi ambazo zitakuwa tayali kukimbia katika maeneo ya matukio kwenye maeneo ya karibu.

“Kutekeleza mradi wa kimataifa wa mawasiliano na uchukuzi katika ziwa Victoria, ambao ni mpana sana, lengo lake ni kuboresha mawasiliano na kusaidia katika shughuli za uokoaji zinapotokea ajali ili watu waweze kuwasiliana, na msaada wa karibu uweze kufika.

“Ziwa letu ni kubwa katika eneo tunalolimiliki, mradi huu umelenga kuwasaida watu wa kawaida kabisa, kwa hiyo Serikali imefanya jitihada kubwa ili kuwafikiria watu wa chini.” Amesema Mlali.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here