Home KITAIFA TARURA KUANZA UJENZI WA DARAJA LA MFILISI-MIKUMI

TARURA KUANZA UJENZI WA DARAJA LA MFILISI-MIKUMI

Google search engine

*Kero ya kukatika kwa mawasiliano katika Kata za Kisanga, Ulaya na Mikumi kumalizika

Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilosa, Mhandisi Harold Sawaki, akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa barabara wilayani Kilosa mkoani Morogoro, mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza wakati wa ukaguzi wa kazi ya ujenzi wa barabara unafanywa na TARURA wilayani hapa

Na MWANDISHI WETU

-KILOSA

WAKALA ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilayani Kilosa imedhamiria kumaliza kero ya muda mrefu ya kukatika kwa mawasiliano katika Kata tatu za Kisanga, Ulaya na Mikumi baada ya kukamilisha taratibu zote za ujenzi wa daraja la Mfilisi litakalokuwa na urefu wa mita 21.75.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi rasmi kazi hiyo kwa  Mkandarasi ili aanze ujenzi, Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilosa, Mhandisi Harold Sawaki amesema kuwa eneo hilo limekuwa changamoto kubwa hasa kipindi cha masika ambapo watu hushindwa kuvuka upande wa pili.

“Mto unapojaa maji mawasiliano hukatika maana kalvati lililopo ni dogo na sasa Serikali imekuja na suluhisho la kudumu la tatizo hili,”amesema Meneja huyo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kasi yake ya kusukuma maendeleo Vijijini kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za miradi.

“Daraja hili linakuja kufungua uchumi wa wananchi na Mhe. Rais anaendelea kuleta fedha nyingi kila eneo iwe barabara, afya, elimu na maeneo mengine na wananchi nyie ni mashahidi wa hili,” amesema Shaka.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Dennis Londo amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali katika kutatua kero za wananchi ikiwemo ujenzi wa barabara na madaraja katika jimbo la Mikumi.

Akiongea kwa niaba ya wananchi, Rehema Mlingwa ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ibegezi amesema kuwa kipindi cha masika eneo hilo huwa linasumbua  maana watu hushindwa kuvuka na hata kuvusha mazao yao na kwamba ujenzi wa Daraja hilo ni mkombozi kwao.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here