Home KITAIFA EWURA yapongezwa kupitia bei za mafuta

EWURA yapongezwa kupitia bei za mafuta

Google search engine

*Ni lengo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuleta nafuu kwa wananchi, Dk. Biteko awataka watumishi EWURA kuzingatia maslahi ya Watanzania

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akizungumza katika Kikao cha Kwanza cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo Novemba 8, 2023 katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square jijini
Dodoma
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akizungumza katika Kikao cha Kwanza cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo Novemba 8, 2023 katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square jijini
Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa EWURA, Dk. James Andilile akizungumza katika Kikao cha Kwanza cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo Novemba 8, 2023 katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury
Square jijini Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko akizungumza katika Kikao cha Kwanza cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (EWURA)

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, ameipongeza hatua hiyo akisisitiza ni nia ya Rais Samia na Serikali kuwaletea nafuu wananchi.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inapitia upya mara kwa mara gharama za uagizaji wa mafuta nchini ili ziwe rafiki zaidi kwa Taifa.

Akizungumza jana wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa EWURA linalofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Doto Biteko amesema hatua ya EWURA imefanyia kazi ushauri wa Rais Samia ili kuleta nafuu kwa wananchi.

Dk.Biteko amesema kuwa, awali zilikuwa kubwa na zilikuwa zikisababisha athari mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa gharama katika Sekta ya Usafirishaji na Uzalishaji.

“Gharama hizi za uagizaji mafuta zilikuwa kubwa mno huku kukiwa hakuna sababu ya kuwa kubwa kwa kiasi hicho, niliwapa maelekezo mkazitazame upya, nashukuru mmeziangalia na ninafurahi kwamba zimeshuka na hivyo kupunguza makali kwa watumiaji”, amesema Dk. Biteko.

Aidha Biteko amewataka Watendaji na Watumishi wa EWURA kuzingatia maslahi ya Watanzania katika kazi zao za Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ili Watanzania wapate huduma bora na kwa unafuu mkubwa.

“Tambueni kuwa Taifa lina mategemeo makubwa na ninyi, hivyo fanyeni kazi zenu kwa weledi na ubunifu mkubwa unaoendana na kasi ya teknolojia na maendeleo ya dunia; kanuni na miongozo yenu mnayotumia katika utekelezaji wa majukumu yenu”amesisitiza Dk. Biteko

Aidha amewataka Watumishi wa EWURA kuweka mkazo kwenye kudhibiti vitendo vya urasimu na rushwa mahali pa kazi, kutoangalia maslahi binafsi wakati wa kutenda kazi.

”Jiepusheni kuwaumiza Watanzania walio wengi,natoa wito kwa wafanyakazi hao kumkemea mtu yeyote anayeonekana kuwa na vitendo vya rushwa na ubinafsi katika eneo la kazi.”amesema

Kadhalika amewataka Wafanyakazi wa EWURA kuwajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha kuwa watoa huduma wanafanya ushindani wenye ufanisi na tija.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here