NA MWANDISHI WETU, MOSHI
BENKI ya NMB imetambia mafanikio makubwa iliyoyapata katika Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro ‘Kili International Marathon 2024,’ zilizofanyika Jumapili ya Februari 25, zikianzia na kumalizikia kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU), mjini hapa.
Zaidi ya washiriki 10,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani, wamekimbia Kili Marathon 2024, mbio zilizohudhuriwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro, waliochuana katika kilomita 42 (full marathon), kilomita 21 (half marathon) na kilomita tano (5km fun run).
Kupitia klabu yake ya mbio za taratibu ‘NMB Jogging Club,’ benki hiyo ilitikisa mbio hizo kupitia washiriki wake zaidi ya 150 – wakiwemo wafanyakazi wa NMB kutoka kanda mbalimbali nchini, kivutio kikubwa kikiwa ni kikundi maalum cha vijana mabalozi wa NMB kiitwacho ‘Chugga Dance’ cha Arusha.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mbio hizo, Meneja Msaidizi wa NMB Jogging Club, Stella Motto, alisema benki yake imepata mafanikio makubwa katika ushiriki wao huo, uliowezesha ‘kuuandegewawili kwa jiwe moja,’ huku akiushukuru uongozi kwa uwezeshaji.
“Tunamshukuru Mungu tumemaliza mbio salama na kimsingitunamshukuru mwajiri wetu NMB kutupa nafasi nyingine ya kushiriki Kili Marathon kwa zaidi ya mwaka wa tano sasa, huku mwaka huu tukipata mafanikio makubwa katika malengo mawili tuliyokuja nayo.
“Tumekuja hapa ili sio tu kujenga mahusiano mema baina ya benki yetu, taasisi shiriki na waratibu, bali pia tulikuwa na malengo mawili ambayo yamefanikiwa sana, nayo ni kujenga na kuimarisha afya za wafanyakazi, lakini pia kunadi moja ya bidhaa zetu sokoni.
“Kupitia washiriki wetu, benki ilichagua kuitumia Kili Marathon 2024 kuinadi bidhaa yetu mpya ya NMB Pesa Akaunti, ambayo ni akaunti nafuu na rahisi zaidi nchini inayofunguliwa kwa Sh. 1,000 tu, na ambayo haina makato ya mwezi kama zilivyo akaunti zingine.
“Tumefanikiwa sana katika maeneo yote hayo, kwa sababu ushiriki wetu ulikuwakivutio na kujenga ‘awareness’ kubwa juu ya NMB Pesa kwa washiriki wengine, lakini pia kwa wananchi walioshuhdia mbio hizo kwenye barabara mbalimbali za mji wa Moshi,” alisema.
Aliongeza kuwa, michezo na mazoezi ni afya na kwamba anaamini ushiriki wao unaenda kuongeza ari ya uwajibikaji kazini, na kuwa uwepo wa washiriki kutoka taasisi na mikoa mbalimbali, pamoja na washiriki bianfsi, unaendakuifikisha NMB Pesa kwa kila Mtanzania kama lilivyo lengo la bidhaa hiyo.
Kwa upande wake, Meneja wa NMB Jogging Club, Shadrack Mijjinga, amejivuniaushirikiwa benki yake katika Kili Marathon, huku akipongeza maandalizi ya taasisi yake, lakini kwa ufanisi wa mbio hizo kwa ujumla wake na kuvutia washiriki mbalimbali.
“Ulikuwamsimu mwingine wa mafanikio makubwa kwetu katika mbio hizi, tulikuwa na maandalizi mazuri yaliyowezesha wengi wetu kukimbia na kumaliza vema kwenye umbali tofauti, wengi wetu tukishirikikilomita 21 na kilomita tano, pamoja na kilomita 42.
“Tunawapongeza waratibu wa Kili Marathon kwa kufanikisha tukio hili kubwa la kimataifa ambalo halikuwa na malalamiko, wala manung’uniko kwa wakimbiaji walioshiriki mbio hizi, hata miongoni mwetu sisi NMB Jogging Club,” alisema Shadrack.
Aliongeza kwa kuwataka Watanzania kuchangamkia akaunti za NMB Pesa ‘Haachwi Mtuuu,’ ili kuwa sehemu ya huduma jumuishi za kifedha, akaunti ambazo zinafunguliwa kidigitali kote nchini kupitia watoa huduma wa benki hiyo kinara nchini.