Home KITAIFA NMB yaunganisha ATM zake na ATM za Benki 17 za Umoja Switch

NMB yaunganisha ATM zake na ATM za Benki 17 za Umoja Switch

Google search engine
Naibu waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (wapili Kushoto) akizindua ushirikiano kati ya Benki ya NMB na kampuni UBX inayosimamia ATM za Umoja switch zinazohudumia Benki zingine 17. Ushirikiano huu utashuhudia wateja wanaotumia kadi za Umoja switch kutumia mashine za kutolea pesa za NMB bila gharama za ziada na wa NMB katika mashine za Umoja switch hivyo hivyo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja Switch, Mariam Malima na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa UBX, Sabasaba Moshingi.

*Ushirikiano huu unaunda mfumo mpana zaidi wa matumizi ya pamoja ya ATM zaidi ya 1,000

Na MWANDISI WETU

-DAR ES SALAAM

BENKI ya NMB na Kampuni ya UBX Tanzania Limited, inayoendesha mtandao wa ATM wa Umoja Switch, ziliingia katika ushirikiano wa kimkakati unaounganisha benki washirika kwenye mtandao mmoja wa ATM.

Ushirikiano huo  wa kimkakati ni hatua muhimu kwa sekta ya kibenki Tanzania kwa kuwa unaunda mfumo mpana zaidi wa matumizi ya pamoja ya mashine za kutolea fedha (ATMs).

Ubia huo wa kimkakati unapelekea kuunganishwa kwa mafanikio makubwa ATM 280 za Umoja Switch na ATM za NMB zaidi ya 700, ikiashiria zama mpya ya upatikanaji wa ATM na ufanisi katika huduma za kibenki nchini.

Kutokana na hali hiyo kupitia ushirikiano huo Watanzania watapata manufaa kadhaa ikiwamo upatikanaji wa huduma za ATM – Wateja wa benkizote 17 za Umoja Switch na wale wa Benkiya NMB wataweza kufanya miamala na kupata huduma za kibenkiwakatiwowotekupitiamtandao wa ATM zaidiya1,000.

Pia kutapunguza gharama ambapo ushirikiano huo unaongeza ufanisi na kwa kiasi kikubwa kuwapunguzia gharama za miamalawateja wa benki zote 17 watakaotumia ATM za NMB nawateja wa NMB watakaotumia ATM za Umoja Switch kwa zaidi ya asilimia 70.

Kuhusu ujumuishi wa kifedha  ubia huo utaongeza matumizi ya kadi kwenye ATM nchini na kupunguza foleni matawini, na hivyo kuwa njia mbadala ya kuimarisha ujumuishi rasmi wa kifedha nchini.

Na kuhusu ufanisi Benki zinazoshiriki zitafikia maeneo ya pembezoni ambayo awali yalikuwa magumu kwa taasisi moja kuyafikia kwa kuweka ATM.

Hata hivyo gharama za uendeshaji atka ushirikiano huo pia utazipunguzia benki shiriki gharama za uendeshaji kayika miamala yote itakayofanyika nchini haitahitajika tena kuchakatwa nje ya nchi, badala yake, hilo litafanywa na mtandao wa NMB na UBX, hivyo kupunguza gharama kubwa za uendeshaji za hapo awali.

Ubia huo ulizinduliwa na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande ambapo amesema kuwa ushirikiano wa NMB na UBX unaongeza thamani kubwa katika juhudi za Serikali za kuongeza idadi ya watu wanaopata huduma rasmi za kifedha kufikia asilimia 85 ifikapo mwaka2025.

Aidha Naibu Chande aliziasa benki nyingine kujiunga na mtandao wa ATM wa NMB na Umoja Switch.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amesema kuwa “Tumefurahishwa na ushirikiano huu kwani unawawezesha wateja wetu kupata huduma za kibenki kwa urahisi. Sasa wateja wetu kwa kujinafasi wanaweza kupata huduma za kibenki kwa unafuu na uhakika kwenye ATM zaidi ya 1,000 kote nchini. Hiyondiyofaidayaushirikianohuu.”

“Ushirikiano huu pia unakwenda kupunguza gharama za uendeshaji kwa benki shiriki kwani miamala yote inayofanyika nchini haitakuwa na ulazima tena wa kuchakatwa nje yanchi,” amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya UBX, Sabasaba Moshingi, amesema kuwa Umoja Switch ilipoanzishwa mwaka 2006 ikiwa na wanachama sita na ATM 30 tu ambazo hazikuweza hata kuwahudumia wateja zaidi ya 2,000. Sasa washirika wa ushirikiano huu wa kimapinduzi  wanaweza na kwa gharama nafuu kuzifikisha kazi za msingi za tawi katika mazingira ya pembezoni kabisa na yenye changamoto.

“Kwa kweli, ushirikiano huu unaashiria dhamira ya pamoja ya kupunguza pengo la kidijitali na kifedha. Kupitia teknolojia na ushirikiano, tunalenga kuwawezesha watu ambao hawahudumiwi vya kutosha na hivyo kuhamasisha ukuaji wa uchumi,” aliongeza.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here