Home KITAIFA Majaliwa awekajiwe la msingi Sekondari ya Dk. Samia

Majaliwa awekajiwe la msingi Sekondari ya Dk. Samia

Google search engine

Na MwandishiWetu,Best Media

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 6, 2023 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili kwa gharama ya Sh bilioni 4 kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambapo Awamu ya kwanza ya mradi huu ulianza tarehe 6 April 2022 na unaotarajiwa kukamilika tarehe 30 Januar 2023 utatumia Sh bilioni 3 na jumla ya majengo 22 yanajengwa

Hadi kufikia Disemba 31, 2022 kiasi cha Sh 2.2 zimetumika katika utekelezaji wa mradi huu. Majaliwa amesema shule hiyo itakapokamilila itapokea wanafunzi 1080 ambapo awamu ya kwanza itapokea wanafunzi 600.

Aidha awamu ya pili ambayo ujenzi wake unatarajiwa kuanza ndani ya mwaka huu kwa gharama ya Sh bilioni 1 inatarajiwa kupokea wanafunzi 480 pale itakapokamilika

Awamu ya pili itahusisha ujenzi wa madarasa 10 yenye ofisi za walimu 3, chumba cha ICT, Maktaba, nyumba 4 za walimu na mabweni 4.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Dk. Samia ameamua kuwekeza kwenye elimu ya mtoto wa kike ili kumpunguzia changamoto zilizowakabili na ndio maana ameamua kujenga shule za wasichana nchi nzima“Si kwamba amemtenga mtoto wa kiume hapana, ameamua kwenda nao wote

Pia, Waziri Mkuu amewataka wakandarasi wanaojenga shule hiyo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa shule hiyo katika muda uliopangwa ili waanze kupokea wanafunzi.

shule ya Sekondari Dk. Samia Suluhu Hassan inatarajia kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano Julai, 2023.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange amesema watahakikisha wanasimamia ujenzi wa mindombinu iliyobaki katika shule hiyo ili ikamilike na ianze kudahili wanafunzi

Akizungumza kuhusu Sekta ya Afya Dk. Dugange amesema kuwa halmashauri zote 184 zitapata magari mawili ikiwa moja ni la wagonjwa (ambulance) na moja ni kwa ajili ya usimamizi wa huduma za afya.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here