*Yasema ni burudani, yabainisha ilivyosajili kampuni 91, mapato yafikia Bilioni 170/
Na MWANDISHI WETU
-BEST MEDIA, DAR ES SALAAM
MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kuhatisha Tanzania (GBT), James Mbalwe, amesema kuwa suala la michezo ya kuhatisha nchini si ajira bali ni burudani
Amesema michezo ya kubahatisha ni michezo kama mingine na haina nia kutaka vijana waharibiwe.
Kutokana na hali hiyo amesema kuwa Serikali kupitia bodi hiyo imekuwa ikifuatilia na kuratibu michezo hiyo kama sehemu ya burudani na imekuwa ikifuatili hatua kwa hatua na wale wanaobainika kuvunja sheria hufutiwa leseni.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari leo Machi 6, 2024 katika mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina nchini, Mbalwe amesema kuwa pamoja na hali hiyo hadi sasa wamefanikiwa kusajili jumla ya kampuni 91 zinazoendesha biashara za aina mbalimbali ya michezo ya kubahatisha nchini.
Amesema kuwa mwendeshaji sharti awe na leseni hai iliyotolewa na Bodi hiyo, na kwamba michezo hiyo hairuhusiwi kuendeshwa katika maeneo yaliyopo Karibu na nyumba za ibada, shule, usalama, yasiyofikika kirahisi na maeneo ya kuendeshea biashara ya michezo ya kubahatisha, na kwamba kwa maeneo yaliyoruhusiwa sharti yawe yamesajiliwa na Bodi hiyo.
“Nina sisitiza michezo ya kubahatisha ni burudani na sio Ajira au njia ya kujitafutia kipato.
“Kwanza ninapenda jamii itambue kwamba michezo ya kuhatisha si uchawi wala si ajira ndio maana inaitwa mchezo wa kubahatisha. Ila hii ni burudani kama zilivyo burudani nyigine za michezo. Nayasema haya kutokana na manganyiko ambao upo kwa baadi ya jamii ambapo wapo wanaodhani hata usipofanyakazi utapata fedha.
“Hapana ni lazima ufanye kazi ili uweze upata fedha ndipo ufanye starehe, ndio maana tunafuatilia kila hatua na wale wanakiuka sheria tunawafuia leseni. Watoto wenye umri chini ya miaka 18 hawarusiwi kushiriki michezo ya kubahatisha kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.
“Mwendeshaji sharti awe na leseni hai iliyotolewa na Bodi, hivyo michezo hii hairuhusiwi kuendeshwa katika maeneo ambayo yamekatazwa kisheria,” amesisitiza Mbalwe.
Ameongeza kuwa, katika Jiji la Dar es Salaam zipo Kasino nane, wakati Arusha na Mwanza kila mkoa zikiwa na kasino moja.
“Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na kasino nane, wakati Mwanza na Arusha kila mkoa una casino moja, sawa na asilimia 90 ya kasino zipo Dar es Salaam,” amesema
Mbalwe, amefafanua kwamba kuna aina mbalimbali ya michezo ya kubahatisha ambayo ni michezo ya kibiashara kama kasino inayochezwa kwenye majumba maalum na mtandaoni, slot inayochezwa zaidi kwenye maduka maalum na baa, ubashiri wa matokeo ya michezo mtandaoni na madukani na bahati nasibu ya jumbe fupi za simu (sms lotteries).
Ameongeza kuwa, mchango wa sekta katika mapato ya serikali kodi imeongezeka kutoka shilingi bilioni 33.6 mwaka 2016/17 hadi kufikia Shilingi Bilioni 170.4 kwa mwaka 2022/23, ambapo ni sawa na ongezeko la wastani wa asilini 407.1 kwa mwaka katika kipindi hicho.
“Sekta ya michezo ya kubahatisha Tanzania tumefanikiwa kuzalisha ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi zaidi ya 25,000. Hivyo sekta hii imefanikiwa kutoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa ajira nchini
“Kazi yetu ni udhibiti, kusimamia na kuratibu uendeshaji wa michezo ya kubahatisha nchini na haifanyi biashara na ipo chini ya Wizara ya Fedha chini ya Msajili wa Hazina,” ,” amesema Mkurugenzi Mkuu huyo
Mbalwe ameeleza kuimarisha ushirikiano katika usimamizi wa sekta na ambapo aliziomba Kamai za Usalama za mikoa kuongeza ushirikiano zaidi katika kudhibiti wavunja sheria ya michezo ya kubahatisha.
Amema kuanzishwa kwa GBT kumewezesha sekta ya michezo ya kubahatisha kuratibiwa vizuri zaidi na iweze kuchangia ipasavyo katika Pato la Taifa na wananchi wanaojishughulisha kwenye michezo hiyo wanalindwa ipasavyo.
“Sekta inakuwa kwa kasi na kwa sababu hiyo kunahitaji uratibu makini ili iendelee kukua katika namna ambayo utaratibu unaopasa bila kupoteza malengo ya msingi ya kuanzishwa kwake,” amesema Mbalwe.
Amesema ajira zilizozaliswa Sekta ya michezo yakubahatisha Tanzania imefanikiwa kuzalisha ajira zilizo rasmi nazisizo rasmi zaidi ya 25,000.