Home KITAIFA WANANCHI WAMETAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA KWA VITENDO KUELEKEA  UCHAGUZI...

WANANCHI WAMETAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA KWA VITENDO KUELEKEA  UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Google search engine
Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni, akizungumza na wananchi katika mkutao wa hadhara uliofanyika eneo la Stende Kuu ya Mabasi mjini Same

Na MWANDISHI WETU

-SAME

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjarfo, Kasilda Mgeni, amewataka waanchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanamuenzi Rais Samia Suluhu Hassan kupitia masanduku ya kura kwa kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye Uchauzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo amesema iwapo watafanya hivyo kwa kukiamini CCM suala la maendeleo litaendelea kuwa wajibu kwa jamii nyakati zote za utawala wa chama hicho kuanzia ngazi za vijiji, kata na majimbo yote nchini.

Kauli hiyo ameitoa leo mjini Same, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Stendi ya Mabasi ajili ya lengo la kusikiliza na kutatua kero na malalamiko mbalimbali ya wananchi.

Amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Same ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Sisi kama viongozi wa Serikali tuliopewa dhamana ya kumwakilisha kwenye maeneo haya tutaendelea kutatua kero na malalamiko yanayowakabili wananchi wetu kwa kufanya mikutano ya hadhara kwenye maeneo yenu na tutaendelea kuwajibika kwa vitendo ili wananchi wetu muweze kuishi kwa usalama na amani kwenye wilaya yetu ya Same,” amesema DC Kasilda

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here