Home KITAIFA WAZIRI MKUU ANGOZA KIKAO CHA WABUNGE KUPOKEA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA UKOMO...

WAZIRI MKUU ANGOZA KIKAO CHA WABUNGE KUPOKEA MAPENDEKEZO YA MPANGO NA UKOMO WA BAJETI

Google search engine
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiogoza kikao cha wabunge wote leo, Machi 11, 2024 kuhusu Mpango wa Maendeleo na Ukomo wa Bajeti. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu na kulia ni Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dotto Biteko

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameongoza mkutano wa wabunge wote wa kupokea Mapendekezo ya Serikali ya Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka fedha 2024/2025.

Mkutano huo umefanyika leo Machi 11, 2024 katika ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.

Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2024/25 yaliwasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Uwekezaji na Mipango,  Profesa Kitila Mkumbo huku Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka fedha 2024/2025 yakiwasilishwa Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Ofisi ya Rais-Uwekezaji na Mipango,  Profesa Kitila Mkumbo akiwasilisha Mpango wa Maendeleo ya Taifa
Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba

Mara ya baada ya kuwasilishwa kwa Mapendekezo hayo, Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kwa niaba ya  Spika aliekeza Kamati ya Kudumu ya Bajeti kuyafanyia kazi Mapendekezo hayo na kuzishauri Kamati za kisekta ipasavyo.

Kwa upande mwingine waheshimiwa wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge takribani 14 wataanza kufanya ziara za ukaguzi wa miradi ya maendeleo nchi nzima.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here