Home KITAIFA MFUKO WA SELF WATOA SHILINGI BILIONI 324 KWA WANANCHI

MFUKO WA SELF WATOA SHILINGI BILIONI 324 KWA WANANCHI

Google search engine

Na SELEMANI MSUYA

-DAR ES SALAAM

MFUKO wa Self umetoa mikopo ya zaidi ya Sh bilioni 324 kwa wananchi 314,055 wa mikoa 30 nchini huku ukijipanga kupanua wigo siku zijazo.

Mfuko pia umesema katika mikopo iliyotoa kiwango cha mikopo chechefu ni chini ya asilimia 10, huku wakijipanga kukabiliana na changamoto ya mikopo kaushadamu.

Hayo yamesemwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo, Mudith Cheyo akizungumza kwenye mkutano wa 53 wa ya taasisi hiyo na wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam, kupitia uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Cheyo amesema hadi Desemba 31 mwaka jana, mfuko huo unaotarajia kuwezesha wananchi wengi kwa mikopo, ulifikia zaidi ya wananchi 300,000; wanawake 166,449 sawa na asilimia 53 na wanaume 147,606 sawa na asilimia 47.

Amesema pia umekopesha na kuzijengea uwezo taasisi ndogo 200 za fedha na kutengeneza ajira 37,024 kwa mwaka jana na kutoa elimu kwa wakopaji 1,519.

Ofisa Mtendaji huyo alisema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan, Mfuko wa Self umepata faida ya Sh bilioni 2 huku ikitoa gawio kwa serikali zaisdi ya shilingi milioni 240

“Tumekuwa tukikua mwaka hadi mwaka, na tumepata faida ya Sh bilioni mbili, tukatoa gawio la zaidi ya Sh milioni 240, huku mtaji ukiongezeka kutoka Sh bilioni 56 hadi 62,” alisema.

Cheyo alisema mikakati yao ni ifikapo mwaka 2026 Mfuko uwe na matawi 20 kutoka 12 ya sasa, huku akisisitiza kuwa wamejipanga kuondoa mikopo kaushadamu.

Amesema kupitia mkakati wa kuongeza matawi wanatarajia kwa siku za karibuni watafikia kundi kubwa la Watanzania hasa kwenye SMEs ambao wanakadiriwa kufikia milioni nne.

Mkurugenzi wa Biashara wa Self, Petro Mataba alisema Mfuko unafanya kazi kwa kuzingatia uadilifu, ushirikiano, ubunifu, mteja na uwajibikaji, hali imewawezesha kukua kwa kasi.

Amesema Mfuko umetoa mikopo kwa wananchi na taasisi kama Kampuni ya Star Natural Product iliyokopeshwa Sh milioni 100 na shule ya Bright Future Academy Sh milioni 400.

Alitaja changamoto zilizopo kuwa ni wananchi wengi kukosa elimu ya fedha, kujishughulisha na biashara zisizo rasmi na kukosa utamaduni wa kukopa na kurejesha, ingawa wanaendelea kutoa elimu ili wabadilike.

Mkurugenzi wa Masoko, Santiel Yona alisema mpango mkakati wao ni kufikia wateja wengi hasa wa kipato cha chini, kuongeza ufanisi na kuhakikisha taasisi inakuwa endelevu.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here