Home KITAIFA MAMLAKA YA AFYA YA MIMEA NA VIUATILIFU TANZANIA YATAJA MKAKATI WA KUKUZA...

MAMLAKA YA AFYA YA MIMEA NA VIUATILIFU TANZANIA YATAJA MKAKATI WA KUKUZA KILIMO, MASOKO NCHINI

Google search engine

*Yavuka lengo la ukusanyaji mapato na kufikia Bilioni 6.1/-, yaendelea na kudhibiti kweleakwele kulinda mazao

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) , imesema kuwa ili kuhakikisha Tanzania inafanikiwa kwenye sekta ya kilimo ni lazima wakulima wakubali mabadiliko ya teknolojia ya kisasa.

Kutokana  mamlaka hiyo imeweka alengo ya kimkakati yenye tija kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habri leo Machi 13, 2024 katika mkutano ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru, amesema kuwa kwa sasa Tanzania inaendelea kupiga hatua kwenye sekta ya kilimo ikiwamo kuwa na mimea ya mazao ambayo yanalindwa kwa kuwa na viuatilifu kwenye ubora.

UTEKELEZAJI NA MAFANIKIO YA SHUGHULI ZA MAMLAKA KWA MWAKA 2023/2024

Profesa Ndunguru, amesema kuwa katika mwaka wa Fedha 2023/2024  Mamlaka hiyo ilikasimia kukusanya kiasi cha fedha cha Sh bilioni 6,454,437,453, mapato ya ndani  na katika kipindi cha miezi mitatu tu yaani Julai  2023 hadi Septemba 2023, ambapo mamlaka imeweza kukusanya kiasi cha Shilingi 6,143,965 337.61 (95.2%) ya makadirio ya makusanyo ya mwaka mzima  kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ya ndani.

“Hii ni dhahiri  kwamba hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha, Mamlaka itaweza kukusanya zaidi ya 100% ya makadirio hayo na hivyo kuweza kuongeza kiazi cha gawio lake kwa serikali kuu (15%) (Government Remitance) kutoka  Shilingi  968,165,000.62 tulizotarajia hadi Shilingi 3,686,379,202.56 kwa mwaka.

“Kwa kipindi cha mwezi Oktoba mpaka Disemba 2023 Mamlaka imekusanya kiasi cha Shilingi 5, 352, 196, 967.04. Kwa kipindi cha Januari mpaka tarehe 6 Machi  2024 Mamlaka imekusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 3.7,” amesema Profesa Ndunguru

MALENGO YA KIMKAKATI YA MAMLAKA

Amesema pia Mamlaka hiyo ina mikakati kadhaa ikiwamo kuimarisha huduma za kupunguza maambukizi ya Ukimwi na magonjwa yasiyoambukiza ikiwa sambamba na utekelezaji wa mikakati ya kudhibiti rushwa

“Kuimarika kwa uwezo wa mamlaka katika kutoa huduma na kuimarika kwa usimamizi na ubora wa Viuatilifu. Kuimarika katika kukidhi matakwa ya biashara ya mazao ya kilimo kimataifa.

“Kuimarika kwa uzalishaji na tija katika Sekta ya Kilimo, kuimarika kwa taarifa za elimu na huduma za kilimo kwa jamii,” amesema

UKAGUZI WA MAZAO

Profesa NduguruamesemaMamlaka imekagua uwepo wa visumbufu katika tani 7,719,418.24 za mazao mbalimbali katika vituo vya mipakani, bandari na viwanja vya ndege yaliyosafirishwa nje ya nchi.

“Vibali vya Kuingiza Mimea Nchini (Plant Import Permit):jumla ya vibali vya kuingiza mimea Nchini Tanzania yalipokelewa na vibali 5201  vilitolewa,” amesema

MAJUKUMU YA MSINGI YA TPHPA

Mkurugenzi Mkuu huyo wa TPHPA, amesema kuwa msingi wa majukumu yao ni kuwezesha masoko ya mimea na mazao ya mimea hapa nchini na kimataifa kwa kufanya ufuatliaji wa visumbufu (Pest surveillance) na uchambuzi wa hatari ya visumbufu (pest-risk analysis (PRA) .

“Kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa usafi wa mimea na mazao mashambani, ghalani  na mipakani (entry and exit points) ili kuzuia kuenea kwa visumbufu. Kudhibiti uagizaji, usafirishaji, utengenezaji, usambazaji, uuzaji, na matumizi ya viuatilifu na vifaa vya unyunyiziaji wa viuatilifu ili kuleta tija katika Kilimo

“Kulinda afya ya binadamu na mazingira kwa usimamizi bora na endelevu wa viuatilifu na afya ya mimea. Kutoa huduma ya utambuzi na uhifadhi wa bioanuai za mimea na vinasaba vya mazao,” amesema Profesa Ndunguru

UTOAJI HUDUMA KWA MFUMO WA KIELECTRONIKI (ATMIS)

Profesa Ndunguru, amesema kuwa mfumo huo ni rafiki kwa wadau wa viuatilifu na afya ya mimea na kuwapunguzia gharama za ziada wateja.

“Utoaji vibali kwa haraka kwa njia ya mtandao, huduma huchukua muda mfupi na malipo yanafanyika kwa njia ya mitandao

“Lakini matumizi haya ya mfumo huu wa malipo umechangia kuwa ongezeko la upatikanaji wa taarifa za wateja pamoja na kubresha maabara za kikemia na kibiolojia,” amesema Profesa Ndunguru

MATEGEMEO YA SERIKALI KUUNDWA KWA MAMLAKA

Mkurugenzi huyo Mkuu wa TPHPA, amesema kuwa hatua ya kuongezeka kwa ufanisi katika shughuli za afya ya mimea na udhibiti wa viuatilifu kutokana na kutumika kikamilifu kwa miundombinu, raslimali watu na vitendea kazi

“Kuongezeka kwa maduhuli ya Serikali, kuongezeka kwa uhakika wa chakula na malighafi ya viwanda  kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo, kupungua kwa madhara ya kiafya kwa binadamu yatokanayo na masalia ya viuatilifu, sumu kuvu, madini zito (heavy metal) na visibika vingine (contaminants) kwenye mazao.

“Kupungua kwa viuatilifu bandia sokoni kutokana na kuimarika udhibiti katika utengenezaji, uingizaji, usambazaji na uuzaji,” amesema

MALENGO YA MAMLAKA 2023/2024

Akizungumzia maleng ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2023/24 ni kuhakikisha wanadhibiti visumbufu vya mimea na mazao vya milipuko na kikarantini.

“Kudhibiti viuatilifu bandia, kuwezesha biashara za mimea na mazao katika masoko ya kikanda na kimataifa. Kuwajengea uwezo wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo kwenye udhibiti wa visumbufu na matumizi sahihi na salama ya viuatilifu na kutoa huduma ya utambuzi, uhifadhi na matumizi endelevu ya  bioanuai za mimea na vinasaba vya mazao,” amesema

USIMAMIZI WA AFYA YA MIMEA

Profesa Ndunguru, amesema kuwa mamlaka hiyo imefanya ukaguzi ili kudhibiti visumbufu vya kikarantini  na jumla vibali  39,230 vya Usafi wa Mimea  vilitolewa na kuwezesha usafirishaji wa mimea, vipando na mazao mbalimbali  nje ya nchi.

Baadhi ya wahariri walioshiriki mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam

UPATIKANAJI WA MASOKO NA VIUATILIFU

Amesema mamlaka imeanzisha kituo (Plant Health and Biosafety Intelligency Unit) chenye jukumu la kuwezesha kufungua masoko na kuyaendeleza masoko ya mazao mbalimbali kitaifa, kikanda na kimataifa na kufuatilia visumbufu vya mimea ili kuvidhibiti kabla havijaleta madhara kwa wakulima.

Majukumu ya Kitengo hicho ni pamoja na uchakataji wa takwimu za mazao na visumbufu zilizopo katika portal kama ATMIS na kutengeneza taarifa kwa ajili ya maamuzi.

“Utambuaji na ubainishaji wa visumbufu kwa kutumia teknolojia ya remote sensing na GIS. Kuwezesha upatikanaji wa taarifa sahihi za savei kwa wakati sahihi kama sehemu ya mchakato wa upatikanaji masoko ya kimataifa.  

“Kuchora ramani za maeneo amabayo ni kitovu cha visumbufu kwa ajili ya ufuatiliaji. Kufanya ujasusi wa aina na mwenendo wa visumbufu katika nchi jirani Tanzania na kutengeneza njia za kujilinda. Matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ukusanyaji wa taarifa, uchakataji wake kwa kutumia mifumo kama ATMIS na hifadhi yake.

“Kituo cha taarifa mbalimbali za mazao kwa wakulima pmoja na ufuatiliaji wa taarifa za masalia ya viuatilifu katika bidhaa za Tanzania, na kuainisha njia za kiteknolojia za udhibiti wake,” amesema

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here