Home KITAIFA WAZIRI AWESO ATUA UFARANSA KUJADILI PROGRAM YA MAJI AWAMU YA PILI CHINI...

WAZIRI AWESO ATUA UFARANSA KUJADILI PROGRAM YA MAJI AWAMU YA PILI CHINI AFD

Google search engine
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akijadiliana jambo na mwenyeji wake, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Ali Jabir Mwadini leo Jijini Paris nchini Ufaransa

Na MWANDISHI WETU

-PARIS, UFARANSA

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, leo Machi 13, 2024 amewasili Paris nchini Ufaransa na kupokewa na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini hapa Ali Jabir Mwadini kwa mwaliko maalum wa Benki ya Maendeleo ya Ufaransa (Agence Française de Développement – AFD).

Katika ziara hiyo, Waziri Aweso atafanya mazungumzo na Waziri wa Nchi-Maendeleo ya Uchumi Ufaransa (Secretary of State for Economic Development), Chrysoula Zacharopoulou, pamoja na uongozi wa Shirika la AFD.

Mazungumzo hayo yatajikita katika uwekezaji na utekelezaji wa awamu ya pili ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Ziwa Victoria katika Jiji la Mwanza ambapo awamu ya kwanza imetekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank) na Benki ya maendeleo ya Ufaransa (AFD) kwa gharama ya takribani Euro Milioni 135.5

Aidha Waziri Aweso atafanya mazungumzo na uongozi wa Benki ya Maendeleo -AFD ukiongozwa na Marie-Hélène LOISON Naibu Meneja Mkuu wa AFD ambapo kwa pamoja watajadili utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati inayoendelea katika miji ya Shinyanga na Morogoro inayofadhiliwa na Serikali ya Ufaransa kupitia Benki yake ya Maendeleo (AFD) kwa gharama ya Jumla ya Euro milioni 145.

Vilevile, mazungumzo hayo yatahusu kupanua wigo wa uwekezaji katika Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira katika Ziwa Victoria awamu ya Pili yenye thamani ya Euro milioni 180.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo wa Maji atashiriki katika mahafali ya watumishi wa Sekta ya Maji katika Chuo cha AgroParsTech kupitia ufadhili wa AFD ikiwa ni pamoja na wakurugezi wa Mamlaka za Maji waliokua wakiongeza ujuzi.

Katika hafla hii inatarajiwa kuwa Aweso atafanya mazungumzo ya kuanzisha ushirikiano kati ya AgroParisTech na Chuo cha Maji.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here