Na MWANDISHI WETU
-PWANI
Wananchi wa maeneo ya Rufiji na Kibiti wanaoishi kando ya Mto Rufiji wameanza kuondoka katika makazi yao baada ya serikali kutoa tahadhari za kuwepo kwa mafuriko yakiambatana na zoezi la kufugua milango ya mradi wa kufua umeme wa maji katika Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amewaambia wanahabari leo Machi 14 kuwa tayari athari za maji kutoka katika bwana zimejitokeza ambapo baadhi ya mashamba ya wananchi yameathirika kwa kuzingirwa na maji.
Kunenge amesema, baada ya maji hayo kufunguliwa, maji hayo yalizingira mashamba na kuharibu baadhi ya mazao ya wananchi na kwamba kwa sasa bado wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa Ili kuthibiti maafa ikiwemo vifo visivyo vya lazima
“Bwawa la Mwalimu Nyerere, limefurika kuliko matarajiyo yaliyo kuwepo,ambapo tulipokea taarifa kutoka wizarani na Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) kwamba wanataka kufungua milango ya Bwawa. Tulitoa taarifa za tahadhari kwa wananchi kuondoka maeneo hayo lakin baadhi hawakufanya hivyo hivyo nasisitiza waondoke katika maeneo hayo,” amesema Kunenge.
Aidha amesema taarifa za kufunguliwa kwa Bwawa hilo zilitolewa kuanzia Machi Mosi mwaka huu na zoezi lilifanyika Machi 05, majira ya saa 9:00 alasiri.