Home KITAIFA MUSEVENI, RUTO WAMFUATA RAIS SAMIA WATETA KUHUSU MTANGAMANO AFRIKA MASHARIKI

MUSEVENI, RUTO WAMFUATA RAIS SAMIA WATETA KUHUSU MTANGAMANO AFRIKA MASHARIKI

Google search engine
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na wageni wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais William Ruto wa Kenya walipowasili Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 14 Machi, 2024.
Kwenye mazungumzo yao wamezungumzia masuala ya mtangamano wa Afrika Mashariki hususan umuhimu wa kuharakisha zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi Juu ya muundo na maeneo ya kuangaliwa katika Rasimu ya Katiba ya Fungamano la kisiasa la Afrika Mashariki (EAC Political Confederation). Zoezi hilo limeshafanyika katika nchi za Burundi, Uganda na Kenya na linatekelezwa na Timu ya Wataalamu inayoundwa na Wajumbe watatu kutoka kila nchi Mwanachama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais William Ruto wa Kenya wakiangalia picha ya Viongozi wa Nchi mbalimbali za Afrika wakati Rais Museveni alipomkabidhi Rais Samia zawadi hiyo baada ya mazungumzo yao Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 14 Machi, 2024.
Kwenye mazungumzo yao wamezungumzia masuala ya mtangamano wa Afrika Mashariki hususan umuhimu wa kuharakisha zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi Juu ya muundo na maeneo ya kuangaliwa katika Rasimu ya Katiba ya Fungamano la kisiasa la Afrika Mashariki (EAC Political Confederation). Zoezi hilo limeshafanyika katika nchi za Burundi, Uganda na Kenya na linatekelezwa na Timu ya Wataalamu inayoundwa na Wajumbe watatu kutoka kila nchi Mwanachama.
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here