Home KITAIFA REA YAJIVUNIA MAFANIKIO LUKUKI MIAKA MITATU YA UONGOZI WA RAIS Dk. SAMIA...

REA YAJIVUNIA MAFANIKIO LUKUKI MIAKA MITATU YA UONGOZI WA RAIS Dk. SAMIA SULUHU HASSAN

Google search engine

* KUGAWA MITUNGI YA GESI TAKRIBANI 450,000 NA KUJENGA MIFUMO YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA TAASISI 100

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

KATIKA Kipindi cha Miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), unajivunia mafanikio makubwa kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Pamoja hali hiyo REA kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Machi 19, 2024 na Kitengo cha Uhusiano kwa Umma na Mawasiliano, ilieleza mikakati na mafanikio lukuki waliyoyapata ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Taarifa hiyo ilieleza baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kuunganisha umeme kwa vijiji 5,481 na kufanya vijiji vyenye umeme kufikia 11,843 sawa na asilimia 96.14 ya vijiji vyote nchini ambavyo ni 12, 318.

Vilevile, vitongoji 5,562 vimefikishiwa huduma ya umeme na kufanya vitongoji vyenye umeme kufikia 32,750 sawa na asilimia 51 ya vitongoji vyote nchini ambavyo ni 64,760.

Aidha, vitongoji vingine 8,150 vitafikishiwa umeme kupitia Miradi ya Ujazilizi kabla ya kuisha mwaka 2025.

“Kwa upande wa nishati safi ya kupikia, hadi sasa REA imewezesha ugawaji wa Mitungi ya Gesi (LPG) na vichomeo vyake 83,500. Vilevile, ndani ya Mwaka wa Fedha 2023/24, REA itagawa kwa bei ya ruzuku, Mitungi ya Gesi takribani 450,000 pamoja na kujenga mifumo ya nishati safi ya kupikia kwa Taasisi 100 zinazohudumia watu zaidi ya 300,”ilieleza taarifa hiyo ya REA

Miradi hiyo ambayo ni endelevu na itatekelezwa kila mwaka ili kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hasan katika azma yake ya kumtua mama mzigo wa kuni, kulinda misitu, kuzuia mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kulinda afya za Watanzania.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here