Home KITAIFA BALOZI KASIKE ATETA NA WAZIRI WA AFYA NCHINI MSUMBIJI

BALOZI KASIKE ATETA NA WAZIRI WA AFYA NCHINI MSUMBIJI

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-MAPUTO, MSUMBIJI

BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Msumbiji, Phaustine Kasike, amekutana na Prof. Armindo Tiago, Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Msumbiji Machi 20,  2024 kwenye Ofisi za Wizara ya hiyo zilizopo Jijini Maputo.

Wakati wa mkutano huo, viongozi hao wawili walizungumza masuala mbalimbali ya Ushirikiano katika Sekta ya Afya ikiwemo pendekezo la kusainiwa Hati ya Makubaliano (MoU) itakayowezesha Tanzania kuuza Madawa na Vifaa Tiiba nchini Msumbiji.

Aidha, Viongozi hao walizungumza pendekezo la Tanzania la kutuma Timu ya Wataalam wa Afya watakaoweka kambi nchini Msumbiji kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wenye matatizo ya moyo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here