Home KITAIFA WANAGDSS WABAINI UPATIKANAJI WA MAJISAFI, JIJINI DAR ES SALAAM BADO CHANGAMOTO

WANAGDSS WABAINI UPATIKANAJI WA MAJISAFI, JIJINI DAR ES SALAAM BADO CHANGAMOTO

Google search engine

Na SHARAFI HAJI

-DAR ES SALAAM

IMEBAINIKA kuwa watu binafsi wamekuwa wakichimba visima vya maji Jijini Dar es Salaam kwa gharama kubwa huku changamot kubwa ikiwani kubaini usalama wa maji hayokama sheria na sera ya maji inavyoelekeza.

Kutokana na hali hiyo imeelezwa kuwa kwa Jiji la Dar es Salaam bado kuna changaoto za uhaba wa maji jambo ambalo limegeuka mzigo kwa wananchi hasa wanawake ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta huduma hiyo.

Akizungumza leo Machi 20,2024 Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)  Lilian Liundi, Makao Makuu ya Mtandao huo Mabibo, Jijini Dar es Salaam, katika semina za Jinsia na Maendeleo(GDSS), ambapo amesema wamebaini kufanyika kwa biashara ya maji hali ya kuwa huduma hiyo ni takwa na haki ya msingi kwa binadamu.

Amesema jambo hilo si sawa kwani ni haki ya mtu na hitaji la msingi kwa binadamu hivyo hayapaswi kuuzwa wanatakiwa kuyapata bure.

“Maeneo ya nchi za wenzetu mtu akitaka maji anaenda tu bombani anakinga anakunywa akitaka ya chupa ni mapenzi yako, swala la kuwa na vizimba kwenye maeneo ya shule na ambayo watu wanaweza kuvifikia linatakiwa kutiliwa mkazo,” amesema Lilian

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa bado kuna vizimba vya maji vimevamiwa na watu wasio na mapenzi mema kwa nchi ambapo ameomba mamlaka husika kuondoa watu hao ili kufufua vizimba hivyo ili wananchi waondokane na kadhia hiyo.

Kwa Upande wake, Diwani wa Kata ya Makurumla Manispaa ya Ubungo, Bakari Kimwanga ameahidi kwenda katika eneo lake na kupambana kutatua changamoto hiyo kwa kuzungumza na viongozi wa juu kuunda nguvu za pamoja kuondoa tatizo hilo.

Naye Mwenyekiti Msaidizi wa Kata ya Majohe Wilaya ya Ilala, Joseph Safari amesema kundi kubwa linaloathirika katika suala la maji ni wanawake ambapo upatikanaji wa huduma hiyo unakadiliwa kuwa ni zaidi ya masaa manne kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

“Tunatamani kujua Serikali imewekeza nguvu yao kiasi gani kwenye maji kwa kuzingatia taarifa na takwimu, tunatamani kuona uwazi wa tafiti ambazo serikali imefanya, ikizitolea majibu ni kiasi gani maji yameingia kwenye jamii na suala la mifumo ya maji safi yaliyopita katika njia ya bomba la maji taka ambapo yakipasuka tunakunywa maji ambayo yamechanganyika na majitaka,tunatamani kupata majibu,” amesema Safari.

Maji yamekuwa ni changamoto endelevu hasa katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na ongezeko la watu nchini katika maeneo ya mjini na vijijini, ambao wanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 60.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here