Home KITAIFA TANTRADE YAPOKEA VIFAA VYENYE THAMANI YA BILIONI MOJA KUTOKA UBALOZI WA KOREA...

TANTRADE YAPOKEA VIFAA VYENYE THAMANI YA BILIONI MOJA KUTOKA UBALOZI WA KOREA KUSINI

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade)  imepokea vifaa mbalimbali kutoka kwa ubalozi wa Korea Kusini vyenye thamani ya Shilingi Bilioni Moja.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kupokea vifaa hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Latifa Khamis amevitaja vifaa walivyopokea ni  vibanda 500 vya kuoneshea maonesho, kompyuta mpakato 10, komputa za kawaida 30, Scana 30 pamoja na Jenereta la KVT 60.

Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Latifa Khamis

Amesema  vifaa hivyo ni muhimu na vya thamani kwa Mamlaka hiyo kwani vitaongeza mapato na kuleta ufanisi katika maonesho ya Biashara ya kimataifa (Sabasaba)

Kutokana na hai hiyo, amesema kuwa katika kuboresha zaidi maonesho ya kimataifa ya Biashara (sabasaba) Tanrade iliuomba ubalozi wa Korea Kusini kupata vifaa ikiwemo vibanda  ambavyo vitasaidia katika kuboresha maonesho kwenda vizuri.

“Kama mnavyoshuhudia kila siku zinavyokwenda wadau wamekuwa wakiitaji kushiriki maonesho lakini wamekuwa wakikosa nafasi hivyo kupitia vibanda hivi tutaongeza washiriki na ufanisi pamoja na kuongeza mapato wa nchi,” amesem Latifa

Mbali na msaada huo pia  amesema wako katika mazungumzo baina ya Tan Trade na Ubalozi wa Korea Kusini yanayolenga zaidi kuboresha Utendaji kazi huku akifafanua mahusiano yao hayaishii Tan trade pake bali na katika maeneo mengine.

Aidha amesema  maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 48 ya mwaka huu yataimarika na yatakuwa yenye mvuto zaidi.

Balozi wa Korea kusini, Kim Sun Pyo

Kwa upande wake Balozi wa Korea kusini, Kim Sun Pyo ameeleza kwamba wataendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali  huku akitoa rai kwa wafanyabiashara wa Tanzania kusafirisha bidhaa zao ili kwenda kuziuza Korea Kusini.

“Upo umuhimu wa kuwahamasisha wananchi wa Korea kusini  waweze kununua bidhaa kutoka Tanzania. Tunahitajika kuhamasisha uhusiano wa pande zote mbili katika masuala haya,” amesema

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here