Home KITAIFA NMB YATOA VIFAA VYA UJENZI KWA SHULE SITA NYASA

NMB YATOA VIFAA VYA UJENZI KWA SHULE SITA NYASA

Google search engine
Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa, Salim Ismalil (katikati) akipokea moja ya mabati kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini, Faraja Ng’ingo (watatu kushoto) katika hafla ya kutoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita za Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa. Jumla ya vifaa vivyo vina thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 29. Wengine ni walimu wa shule nufaika pamoja na wafanyakazi wa Benki ya NMB.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa, Salim Ismail akiwakabidhi mabati walimu wakuu kutoka shule sita wilayani Nyasa (walio kulia) ambazo ni mchango wa benki ya NMB katika kutatua changamoto za uezekaji katika shule hizo. Jumla ya mabati hayo na vifaa vingine vya uezekaji vina thamani ya Shilingi milioni 29. Wapili kulia ni meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kusini, Faraja Ng’ingo.

Na MWANDISHI WETU

-RUVUMA

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 29.7 kwa shule sita zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo iliyofanyika katika shule ya msingi Nangombo mjini Mbambabay, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini, Faraja Ng’ingo amevitaja vifaa vilivyotolewa na Benki hiyo kuwa ni mabati na misumari kwa ajili ya kuezekea.

Amezitaja shule zilizonufaika na msaada huo ni shule tano za msingi ambazo ni shule ya Nangombo iliyopata vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni tano, shule ya Chiwindi vifaa vya milioni 4.6, Lundo vifaa vya milioni 4.5, Chinula vifaa vya milioni 4.28, Ndingine vifaa vya milioni 6.9 na Shule ya Sekondari moja ya Ngumbo ambayo imepewa vifaa vya milioni 4.28.

“Vifaa hivi tunavyokabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya  jamii,sisi kama Benki tunaowajibu  wa kuhakikisha jamii inayotuzungukainafaidika kutokana na faida tunayoipata,’’ amesema Ng’ingo.

Amesema kwa miaka kadhaa NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi kwenye miradi ya elimu kwa kutoa madawati na vifaa vya kuezekea na sekta ya afya vifaa vya magodoro,vitanda na vifaa vingine vya kusaidia matibabu.

Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyasa, Salum Ismail ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa vifaa hivyo ambapo amesema benki hiyo imekuwa inatoa misaada mbalimbali serikalini katika sekta za elimu na afya.

Amesema benki hiyo pia imekuwa inatoa mchango mkubwa kwenye majanga ambapo katika Wilaya ya Nyasa, NMBimeshiriki kutoa vifaa vya hurumayakiwemomajeneza kwa watu tisa waliopoteza Maisha hivi karibuni kwa ajali ya gari katika Kata ya Lumeme.

Ametoa rai kwa walimu wa shule ambazo zimekabidhiwa vifaa hivyo vya kuezekea kuhakikisha vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ambapo pia amewataka wazazi na walezi kuendelea kusimamia maadili na nidhamu ya watoto  wao tangu wakiwa nyumbani.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Pasifiki Mhapa amesema NMB imekuwa karibu sana na jamii katika kuhakikisha kuwa changamoto za elimu na afya zinapatiwaufumbuzi.

Hata hivyo amesema mahitaji ya kielimu katika halmashauri hiyo bado ni makubwa kutokana na idadi ya watoto wanaokwenda shule kuongezeka hivyo halmashauri inahitaji wadau kama NMB kusaidia katika maendeleo ya elimu.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wa wakuu waliopata msaada wa vifaa hivyo, Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi  Chinula, Mwl. Emanuel Chilwa ameishukuru NMB kwa msaada huo  ambao unakwenda kupunguza changamoto ya vifaa vya ujenzi katika shule hizo.

Benki ya NMB ina matawi zaidi ya 231 nchini,ikiwa na mashine za kutolea fedha (ATM) zaidi ya 715 nchi nzima,wakala Zaidi ya 30,000 na wateja zaidi ya milioni sita.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here