Home KITAIFA WADAU MSD WAHIMIZWA KUSIMAMIA MATUMIZI SAHIHI YA TAKWIMU BIDHAA ZA AFYA

WADAU MSD WAHIMIZWA KUSIMAMIA MATUMIZI SAHIHI YA TAKWIMU BIDHAA ZA AFYA

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-MTWARA

WADAU wa afya wa Bohari ya Dawa (MSD), Mkoa wa  Mtwara wamehimizwa kusimamia matumizi sahihi ya takwimu za mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya ili ziwawezeshe kufanya maamuzi sahihi juu ya bidhaa hizo katika maeneo yao.

Akifungua kikao cha wadau na wateja wa MSD Kanda ya Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Masasi,  Lauteri Kanoni amesema uwepo wa takwimu sahihi unaiwezesha MSD kuagiza kwa usahihi bidhaa za afya na kuboresha upatikanaji wa bidhaa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha, amewashauri MSD kuhakikisha utaratibu wa vikao  vya mwaka vya wadau ni muhimu kwa pande zote mbili, yaani Bohari ya Dawa (MSD) yenyewe na wadau ili kwa pamoja kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya, kwa kujadili changamoto na kuzitafutia utatuzi.

Kwa upande wake Meneja Kanda ya Mtwara,  Tea Malay ameeleza kuwa kwa sasa kanda ya MSD Mtwara inahudumia vituo vya kutolea huduma za afya 631, na inasambaza bidhaa za afya kila baada miezi miwili.

Naye Meneja Huduma kwa Wateja na Miradi, Dk. Pamella Sawa ameeleza kuwa vikao vya MSD na wadau wake kuanzia sasa vitakuwa endelevu kila mwaka.

MSD Kanda ya Mtwara inahudumia mikoa ya Lindi,Mtwara na Wilaya ya Tunduru.

Wakati huo huo, Halmashauri ya Mji wa Masasi, mkoani Mtwara wameitambua Kanda ya MSD Mtwara kwa kuboresha huduma za afya, hasa katika jukumu la msingi la kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya umeimarika katika Halmashauri hiyo.

Tuzo hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Masasi, Dk. Salum Gembe kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here