Home KITAIFA JAMII IJENGE UTAMADUNI WA KUPIMA KIFUA KIKUU, KUPATA USHAURI

JAMII IJENGE UTAMADUNI WA KUPIMA KIFUA KIKUU, KUPATA USHAURI

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

KUELEKEA siku ya Kifua Kikuu Duniani jamii imeaswa kujijengea tabia kwenda katika vituo vya afya kupima pindi wanapobaini kuwa na dalili za kifua kikuu ili kupatiwa ushauri wa kitaalamu kwani kufanya hivyo kutasaidia kujitambua na hivyo kuanza kupatiwa matibabu ya haraka ambayo hutolewa bure nchini kote badala ya kuhusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam,  Dk.Saudan Masawe alipokua akizungumza ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani inayotarajia kufanyika kila ifikapo Machi 24 ya kila mwaka.

Dk. Saudan amesema watu wengi wenye dalili za kifua kikuu wamekua wakichelewa kufika katika vituo vya afya ili kupima afya zao kutokana na kuhusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina hali inayosababisha afya zao kudhoofika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuamini kuwa wamerogwa na hivyo kutumia muda mwingi kwenda kwa waganga.

Aidha ametoa mwito kwa wananchi kutowanyanyapaa watu wenye kifua kikuu kwani ugonjwa huo unatibika kirahisi endapo mgonjwa atawahi kupatiwa matibabu kwa haraka na kwamba si kila mwenye kifua kikuu ana virusi vya Ukimwi (VVU).

Katika kuhakikisha Hospitali ya Rufaa Mwananyamala imejipanga kukabiliana na ugonjwa kifua kikuu nikatembelea vitengo mbalimbali na kujionea hatua zinazochukuliwa tangu mgonjwa anapoanza matibabu kama inavyoelezwa na wataalamu hao.

Mmoja wa wagonjwa wanapata matibabu ya Kifua Kikuu katika Hospitali hiyo Cornel Malimali wameeleza kuhusu mabadiliko makubwa ya afya yake tangu walipoanza matumizi ya dawa.

Siku ya kifua kikuu duniani mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo “KWA PAMOJA TUNAWEZA KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU”

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here