Vyama vitatu vya upinzani vimetaka uchaguzi wa Nigeria ufutiliwe mbali na kurudiwa, kwa madai ya kuwepo kasoro nyingi.
Chama cha Peoples Democratic Party (PDP), Labour na African Democratic Congress (ADC) vilitoa tangazo hilo katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu, Abuja.
Waliikosoa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (Inic) na jinsi inavyoshughulikia mfumo wa kielektroniki wa kupiga kura.
“Nina madai juu ya udanganyifu huu wa uchaguzi ufuwe kabisa na tunatoa wito kwa INEC kufanya uchaguzi mpya ndani ya kipindi cha dirisha kilichotolewa na sheria ya uchaguzi,” Julius Abure, mwenyekiti wa Chama cha Labour alisema.