Home KITAIFA WAZIRI MAVUNDE ATATUA MGOGORO WA WACHIMBAJI MADINI MALERA-TARIME

WAZIRI MAVUNDE ATATUA MGOGORO WA WACHIMBAJI MADINI MALERA-TARIME

Google search engine

*AONDOA ZUIO LA AWALI LA MGAO WA MAWE, WACHIMBAJI WAISHUKURU SERIKALI KWA UTATUZI WA MGOGORO NA WENYE LESENI ZA KUCHIMBA DHAHABU

Na MWANDISHI WETU

-MARA

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde amefika katika eneo la Malera Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wamiliki wa leseni na Kampuni ya KIRIBO ambao ulipelekea zuio la mgawo wa mawe mpaka baada ya utatuzi wa mgogoro huo.

Waziri Mavunde ametumia takribani saa sita leo Machi 25, 2024 kutatua mgogoro husika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, watendaji wa wizara na viongozi wa wachimbaji wadogo mkoa wa Mara (MAREMA)

“Ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan juu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali katika sekta hii ya madini ambayo inadhoofisha kukua kwa uzalishaji wa madini,” amesema Mavunde

Aidha, amezipongeza pande zote kwa kuridhia makubaliano katika hatua ya awali ya kutatua mgogoro huo.

Ameongeza kwamba kwa kuwa kulikuwa na zuio kwamba mgao wa mawe yaliyozalishwa usimame kwasababu ya mgogoro huu, ameelekeza  zuio hilo liondolewe na mgao wa mawe uanze kesho Machi 26, 2024

“Pia, hakikisheni katika utekelezaji wa wa maridhiano haya,  wachimbaji wadogo hawaondolewi katika eneo hilo na waachwe waendelee na shughuli zao,” amesema Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mtanda amemshukuru Waziri Mavunde kwa kufanikisha utatuzi wa mgogoro husika na kupongeza hatua za kuruhusu mgao wa mawe kwa kuwa hali ya kipato ya wananchi wa eneo hilo ilikwenda chini na mapato ya serikali kutopatikana kwa wakati.

Zaidi ya watu 2000 wananufaika na mgodi huo ambao umekuwa ni shughuli kubwa ya kiuchumi ya wananchi wa Malera.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here