WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameipongeza Benki ya NMB kwa juhudi zao katika shughuli mbali mbali za maendeleo hapa nchini.
Waziri Majaliwa amesema hayo alipotembelea Banda la Benki hiyo wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa iliofanyika katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
” Naipongeza sana benki ya NMB kwa kutoa faida katika benki yao na kuthamini na kuweza kufadhili tukio hili la kitaifa linalogusa maslahi ya wengi” amesema Waziri Majaliwa.
Naye Ofisa mkuu wa wateja wakubwa na Serikali wa benki ya NMB Alfred Shao alisema benki ya NMB inaunga mkono juhudi za Serikali za utoaji wa Elimu ya Usalama Barabarani.
“Sisi kama benki ya NMB tunatoa Elimu ya usalama barabarani kupitia mabango mbali mbali, na pia kupitia makava ya magari tunaandika maneno kama vile funga mkanda, una overtake, Umebima ” alisema Shao.
Shao aliweka wazi kuwa ni mara ya pili sasa wanadhamini wiki ya nenda kwa usalama barabarani . Amewaomba madereva wa vyombo vya moto kuzingatia Sheria za barabarani na kuwa na bima stahiki.
“NMB itaendelea kuwa karibu na jeshi la Polisi
Polisi katika utoaji wa elimu ya usalama barabarani ” amesema Shao.
Shao alisema benki ya NMB inatoa elimu kwa watu wote wa vyombo vya usafiri wa moto na benki yao inakata bima katika matawi yao yote.
“Kwenye kila tawi wetu tunatoa huduma ya Bima kwa kushirikiana na wadau wa karibu Sanlam Life Tanzania ili kuhakikisha watanzania wanapata Bima” alisema Shao.
Afisa mkuu wa fedha Sanlam Life Tanzania Mika Samwel alisema wateja wao wanapopata ajali wanalipwa kwa wakati. Alisema kampuni yao inatoa elimu ya bima kwa kushirikiana na benki ya NMB. Alisema wamefanikiwa kuwalipa wahanga wote wa ajali ya Precision air waliokuwa wamepata ajali katika ndege ya Precision mkoani Kagera.
Naye Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Ramadhani Nganzi ameishukuru benki ya NMB kwa kujitolea kwa hali na mali kuunga mkono juhudi za jeshi la Polisi katika kutokomeza ajali za barabarani.