Home KITAIFA ZAIDI YA MABWAWA 100 YA UMWAGILIAJI KUFANYIWA USANIFU

ZAIDI YA MABWAWA 100 YA UMWAGILIAJI KUFANYIWA USANIFU

Google search engine
Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

TUME ya Taifa ya Umwagiliaji imeishukuru Serikali kwa kuongeza bajeti kiasi cha Shilingi bilioni 403.8 kwa aajili utekelezaji wa miradi  ya umwagiliaji nchini.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa amesema kuongezeka kwa fedha Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itasaidia kufikia malengo ya Taifa ya mchango wa asilimia kumi kwenye Pato la Taifa kupitia kilimo unapatikana .

Aidha alisema Tume imejipanga kufanya utekelezaji wa ujenzi miundombinu ya umwagiliaji na kufanya usanifu wa mabwawa zaidi ya 100 ili kuvuna maji kumsaidia mkulima kulima zaidi ya mara moja na kufanya usimamizi madhubuti kwenye miradi.

Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameipongeza Tume ya Taifa ya umwagiliaji kwa usimamizi madhubuti miradi ya umwagiliaji ambayo ipo kwenye utekelezaji na kukiri kuwa utekelezaji wa miradi hiyo utainua vipato vya wakulima kwa kuwa watalima kwa zaidi ya msimu mmoja wa kilimo.

Hata hivyo Raymond Mndolwa amesema kuwa uwekezaji unaofanywa na serikali katika Tume ya Taifa ya Umwagiliaji utaleta tija kwa wananchi kwa kuwa serikali inachimba visima kwenye halmashauri zote nchini pamoja na kuweka miundombinu ya umwagiliaji ili wakulima waweze kulima kwa mwaka mzima.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here