MADENI KWA VYOMBO VYA HABARI SASA KULIPWA
Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa madeni ya vyombo vya habari kwa Serikali ambayo ameahidi na kuagiza kufanyiwa kazi isizidi Desemba mwaka huu.
Amevitaka vyombo vya habari vinavyodai madeni hayo kuwepo na ushahidi wa kutosha mana anataarifa madeni mengi hayana ushahidi na waandishi wenyewe walikiri katika eneo hilo.
Rais Dk Samia amehuzunishwa na hali ya uchumi inayowakabili mwandishi wa habari mmoja mmoja na kwenye vyombo vyao haswa suala zima la mikataba ya ajira.
Kutokana na hali hiyo amewataka wamiliki wa vyombo vya habari nchini pindi watakapolipwa madai yao na wao pia waweze kuwalipa waandishi wao fedha wanazodai ikiwemo mishahara sambamba na kuwapa mikataba.
UZALENDO KWA NCHI
Rais Samia pia alitumia jumuiko hilo la kongamano hilo la sekta ya habari nchini, kuwakumbusha waandishi wa habari nchini kuwa wazalendo kwa kuripoti habari za Taifa kwa weledi na kutangaza maendeleo yaliyofikiwa.
Amesema vyombo vya habari ni muhimu katika kulisemea Taifa mambo mazuri, lakini kuna baadhi ya waandishi wa habari na v yombo vya habari vimekuwa vikiandika habari za kulitangaza vibaya Taifa lao.
Rais Samia amesema vipo vyombo vya habari vinafanya vizuri na kuitangaza Tanzania kwa kazi nzuri lakini kuna vingine hasa mitandao ya kijamii vimekuwa vikipotosha baadhi ya mambo.
“Nikienda huko nchi za wenzetu napongezwa kwa kazi nzuri inavyofanywa kwa kusimamia sekta ya habari, lakini wanahabari wenyewe wapo wasioona mazuri yanayofanywa na Serikali,” amesema Rais Samia