Home KITAIFA CHADEMA KUFANYA MIKUTANO 105 KWA CHOPA

CHADEMA KUFANYA MIKUTANO 105 KWA CHOPA

Google search engine
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Na MWANDISHI WETU

-ARUSHA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinatarajia kufanya mikutano 105 katika mikoa minne ya Kanda ya Kaskazini katika Operesheni yake ya kukijenga chama huku wakitarajia kutumia ndege ‘chopa’ katika ziara hizo.

Akizungumza leo Juni 20, 2024, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa amesema mikutano hiyo itafanyika katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro.

Amesema operesheni hiyo ya siku 21 itafanyika katika majimbo 35 yaliyopo kwenye mikoa hiyo na itaongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.

Amesema katika majimbo ya Ngorongoro na Karatu kutafanyika mikutano mitano kila jimbo na itaongozwa na Mwenyekiti Mbowe na Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Tundu Lissu.

“Kwa majimbo ya Ngorongoro na Karatu tunatarajia kufanya mikutano mitano katika majimbo hayo, na kwa upekee Mwenyekiti wa Taifa atashirikiana na Makamu Mwenyekiti Lissu,.” amesema.

Kutokana na hali hiyo, Golugwa amesema operesheni hiyo inatarajiwa kuanza Juni 22, 2024 katika Jimbo la Karatu mkoani Arusha, ambapo katika majimbo mengine itaongozwa na Mbowe na Mwenyekiti wa Chadema Kanda hiyo, Godbless Lema.

Aidha, amesema kwa sasa wanaendelea kukamilisha maandalizi ya operesheni hiyo ambayo pia watatumia chopa.

Amesema kuwa mikutano hiyo itakuwa na Kaulimbiu yao kwa kuionyesha CCM na wapinzani wao wengine kwamba wana watu; “tuna watu, tuna Mungu, tuna nguvu. Hiyo ndiyo fahari yetu na uimara wetu Kanda ya Kaskazini ambayo ni ngome ya Chadema,”  amesema

Amesema kwa sasa wanaendelea na maandalizia ikiwemo kupeleka barua ya vibali vya mikutano, ndege kuruka na masuala mengine.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here