Home KITAIFA NEMC YAHIMIZA WAWEKEZAJI KUEPUKA ATHARI KWA JAMII NA MAZINGIRA

NEMC YAHIMIZA WAWEKEZAJI KUEPUKA ATHARI KWA JAMII NA MAZINGIRA

Google search engine
Mkurugenzi Mkuu-NEMC
Dkt. Immaculate Sware Semesi

Na MWANDISH WETU

-DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),  limewataka wenye miradi ya maendeleo kufanya kaguzi binafsi kila mwaka baada ya kupata cheti cha mazingira ili kujitathmini mwenendo wa uendeshaji mradi na utekelezaji wa masharti ya cheti hicho.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam  na Meneja wa NEMC – Kanda ya Temeke  Arnold Mapinduzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua zinazofuata baada ya mwenye mradi wa maendeleo kupata cheti cha Mazingira ambapo moja ya masharti ni kufanya ukaguzi binafsi kila mwaka na kuwasilisha taarifa kwa Baraza.

Mapinduzi alisema baada ya mwenye mradi wa maendeleo kupata cheti cha mazingira, Sheria inamtaka kufanya ukaguzi binafsi kila mwaka na kuwasilisha taarifa hizo kwa Baraza ili kufanya tathmini ya uendeshaji wa mradi na utekelezaji wa masharti aliyopewa yenye dhumuni la kulinda na kutunza mazingira.

“Baada ya mwekezaji kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) na kupata cheti cha Mazingira, Sheria inamtaka kufanya ukaguzi binafsi wa mradi wake kila mwaka na kuwasilisha taarifa hiyo Baraza.

“Lengo kujitathmini mwenyewe katika uendeshaji wa mradi wake, kuhakikisha kuwa utekelezaji wa masharti ya cheti cha Mazingira kuwasilisha taarifa hiyo ili Baraza kuona kama kuna changamoto liweze kumsaidia kwa Ushauri,” alisema Mapinduzi.

Akizungumzia kuhusu kaguzi binafsi za mazingira za kila mwaka, Mapinduzi alisisitiza wenye miradi kujikagua na kuwasilisha taarifa sahihi kwa Baraza ili zipitiwe na kutoa ushauri sawia utakaowezesha kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kwa wawekezaji wenyewe na kwa jamii.

Naye, Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Irene John alipozungumza alisisitiza kuwa Baraza litaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kaguzi binafsi za Mazingira baada ya kuanza kwa mradi ili kulinda viumbe hai na Mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo na hivyo kuwezesha maendeleo endelevu ya jamii na Taifa letu kwa ujumla.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here