NA MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kesho anatarajiwa kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho tawala kitakachofanyika Jijini Dar es Salaam.
Taarifa iluyotolewa leo na chama hicho tawala haikuweka wazi ajenda zitakazojadiliwa ingawa baadhi ya wachambuzi wa siasa nchini wanadokeza kwamba huenda kikao hicho kikajadili masuala kadhaa ikiwamo hali ya kisiasa nchini hasa baada ya nia ya kiongozi huyo wa nchi kuonyesha nia yake ya kuunganisha Taifa kwa kuwakutanisha pamoja viongozi wa vyama vya upinzani ksa lengo la kutafuta muafaka wa kitaifa.
Pamoja na hali hiyo wakati kikao hicho cha ngazi ya juu cha CCM kinaketi pia Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa uamuzi katika kesi iliyofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Joran Bashange ya kupinga suala la wagombea wa nafasi za uenyekiti wa mtaa, udiwani na ubunge kupita bila kupingwa katika chaguzi zijazo ambapo jambo hilo huenda likawa ni moja ya ajenda katika kikao hicho katika kuona hali ya kisiasa nchini.