Home KIMATAIFA Rais wa zamani wa Kosovo Hashim Thaci akana mashtaka ya uhalifu wa...

Rais wa zamani wa Kosovo Hashim Thaci akana mashtaka ya uhalifu wa kivita

Google search engine

Rais wa zamani wa Kosovo Hashim Thaci amekana mashtaka 10 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Alisomewa mashitaka siku ya Jumatatu na washtakiwa wenzake watatu, wanaotuhumiwa kwa mauaji ya karibu watu 100 na ukatili mwingine ikiwa ni pamoja na kutoweka kwa lazima.

Madai hayo ni ya tangu vita vya uhuru vya Kosovo dhidi ya Serbia mwaka 1998-99 ambapo zaidi ya 10,000 walikufa.

Bw Thaci alikuwa mwanzilishi mwenza wa kundi linalopigania uhuru na anachukuliwa kuwa shujaa huko Kosovo.

Jeshi la Ukombozi la Kosovo (KLA) lilianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1990 kama kikundi cha wapiganaji wa kabila la Albania, katika eneo ambalo wakati huo lilikuwa mkoa wa Serbia, na wakati wa vita inadaiwa kufanya mashambulizi dhidi ya kabila la wachache la Serb katika eneo hilo.

Wakati Kosovo ilipotangaza uhuru wake mwaka wa 2008, Bw Thaci alikuwa waziri mkuu wake wa kwanza na baadaye rais, lakini alijiuzulu mnamo 2020 kujibu mashtaka huko The Hague.

Waathiriwa na makundi ya haki za binadamu yanatumai kesi yake – katika mahakama maalum inayojulikana kama Chumba cha Wataalamu wa Kosovo – itafichua kilichotokea kwa baadhi ya maelfu ya watu waliotoweka wakati wa mzozo wa Kosovo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here